DALILI ZA MTU ALIYE ATHIRIWA NA MCHEZO WA KUBETI

1. Anatumia muda mwingi kwenye kubeti.
2. Msiri juu ya tabia zake za kubeti na anakuwa mkali akifuatiliwa.
3. Anaongeza dau la kubeti ili atimize shauku yake.
4. Anajitahidi kuacha au kupunguza tabia hii ya kubeti bila mafanikio.
5. Hatulii pia hana raha kama hajabeti.
6. Anabeti akiwa amekasirika,akiwa na mfadhaiko, hanaraha au akiwa na hatia.
7. Anabeti mara nyingi ili arudishe fedha alizopoteza.
8. Muongo, Anadanganya familia yake na marafiki zake juu ya kiwango chake cha kubeti.
9. Anahatarisha maisha yake, anapoteza marafiki,anapoteza kazi, anapoteza fursa au elimu kutokana kubeti.

Ukimuona mtu anadalili hizi tafadhari mpatie ushauri nasaha juu ya tabia yake.
SIFA 10 ZA MTU ANAYE BETI KWA KUWAJIBIKA

1.Beti kwa kujifurahisha.
2.Chukulia pesa uliyopoteza kama gharama ya kujifurahisha.
3.Weka kiwango cha fedha kwa ajili ya kubeti na usizidishe kiwango hicho mfano 15,000 kwa mwezi.
4.Tenga muda maalum kwa ajili ya kubeti na usizidishe muda huo mfano Dakika 20 kwa siku.
5.Kubali kushindwa / kuliwa kama sehemu ya mchezo.
6.Usikope pesa kwa ajili ya kubeti.
7.Usikubali kubeti kuingilie familia yako, rafikizako au kazi yako.
8.Usibeti ili urudishe pesa ulizo poteza.
9.Usitumie mchezo wa kubeti kama faraja ukiwa na mtatizo au umekasirishwa
10.Zijue dalili za mtu aliye athirika kutokana na kubeti

Tafadhari sambaza ujumbe huu kwa vijana wote wanaojihusisha na mchezo huu wa kubeti ili wapate elimu hii.

Imeandaliwa na Koplo 2018

Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.