JINSI YA KUPANGA BAJETI KWA KIDOGO ULICHONACHO
1. Kujua ni vitu gani utakavyokuwa unafanya na hela yako/kujua matumizi ya pesa unapojua utaipata.
2. Kuacha matumizi/manunuzi yasiyo ya lazima mf. kunywa soda/bia nyingi kwa siku na kutoa ofa zisizo na msingi, kununua chai kwenye mighahawa wakati unaweza kupata ofisini/au nyumbani, kula ovyo barabarani hata kama huna njaa.
3. Andaa orodha ya vitu unavyotaka kununua kabla hujaenda sokoni/dukani/store na kujikita katika orodha yako tuu.
4. kupunguza matumizi ya umeme/maji mf. kutokuacha redio/tv inawaka siku nzima, laptop kwenye charge wakati hautumii n.k na kufungulia maji kwa kasi ndogo, kutengeneza bomba za maji zinazovuja, kuoga kwa kutumia shower na kujifunga kuoga haraka si lazima utumia dk 30 bafuni.
5. kupunguza matumizi ya simu kwa kutokupiga simu zisizo na ulazima, unaweza kujiunga na vifurushi vya gharama nafuu kwa siku/wiki hata mwezi lakini kama hamna ulazima usijiunge, sa nyingine mtu haitaji simu inapita hata wiki hana matumizi nayo.
6. kwa wenye magari kupunguza gharama za mafuta kwa kuendesha taratibu, kupunguza mizunguko isiyo na tija kisa una gari, mda mwingine unaweza kutumia usafiri wa dala dala kwenda sehemu panapofikika kwa urahisi(treni ya mwakyembe imesaidia wengi tunasubiri mabasi ya mwendo kasi).
7. Punguza starehe zinazogharimu mf. kwenda movie kila siku m.city, bia samaki samaki 4000.
8. Nunua vyakula vya bei rahisi sokoni na kuhifadhi nyumbani (kwa fresh food nunua kiasi visije kuharibika), pika kwa kiasi kinachotosha na kikibaki hifadhi(usitupe chakula wala usisaze), unaweza kwenda ofisini na lunch box yako kubana matumizi.
8. Tumia kwa uangalifu sabuni za kufulia na kuogea kiasi kidogo kinatosha, nunua bidhaa utakazokua unatumia tuu mf. kuna watu wana aina 6 za perfume tena za gharama, kununua kitu na kukihifadhi haina maana na ni upotezaji wa pesa.
9. jiunge kwenye bima mbali mbali mf. za afya,maisha, nyumba, gari zenye manufaa kwako na fanya uchunguzi kabla ya yote bila kusahau mifuko ya pension.
10. Nunua vitu vilivyotumika (used stuffs), kwa namna fulani vinapunguzo la gharama mf. gari, tv, baiskel, laptop lakini viwe katika hali nzuri inayoridhisha.
11. lipa bili zako kwa wakati, bila kusahau madeni uliyokopa kwa watu, ukiona unazidishiwa gharama kwenye bili zako uliza usilipie kitu ambacho hujatumia kwa uhalali bila kusahau chenji kwa mabaa medi iwe mwisho.
12. unapoona fursa yoyote itakayokupunguzia gharama itumie ipasavyo usisite kuomba punguzo la bei hata kama ni supermarket na fixed bei zao, kuwa mbishi.
13. Acha kabisa matumizi ya vitu/vilevi vya gharama vitakavyokufanya kuwa mtumwa mf. madawa ya kulevya, pombe, sigara.
14. Wekeza pesa katika biashara yoyote kujiongezea kipato na pia usisahau kuweka akiba benki, akiba haiozi.
Leave a Comment