HIFADHI YA SERENGETI YATWAA TUZO YA UBORA AFRIKA
Hifadhi ya Taifa Serengeti imeshinda tuzo ya kuwa hifadhi bora kwa Bara la Afrika kwa mwaka 2019, tuzo iliyotolewa jana na Taasisi ya World Travel huko nchini Mariutius.
Hii ni ya pili kwa Hifadhi hiyo ya Serengeti kutangazwa kuwa hifadhi bora Afrika baada ya mwaka jana 2018 kushinda tuzo hizo kupitia mtandao maarufu wa safari za utalii dunia wa safaribooking.com . Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, washindi katika tuzo hizo za WTA hupigiwa kura na wabobezi katika masuala ya safari na utalii duniani kote.
Wengine walioingia katika kuwania tuzo hizo ni pamoja na Hifadhi za Taifa za Central Kalahari ya nchini Botswana, Hifadhi ya Taifa ya Etosha ya nchini Namibia, Hifadhi ya Taifa ya Bonde la Kidepo Uganda, Hifadhi ya Taifa ya Kruger nchini Afrika kusini na Hifadhi ya Taifa ya Masai Mara ya Kenya.
Leave a Comment