JE, NINI KITATOKEA TIKIAMUA KILA MKOA UJITEGEMEE KWA MAPATO YAKE?


Kwa sasa Tanzania kila mkoa una vyanzo vingi sana vya mapato, na kila mkoa unaonekana umesheheni kila aina ya utajiri. Swali ni Je tukiamua kila mkoa ukusanye kodi zake na kufanya matumizi yake kwa maendeleo ya Mkoa husika ni nini kitatokea?

Najaribu tu kufikiri, kwa sababu inaonekana Makusanyo ni mengi lakini ya yakifika Serikali kuu, yanakwama na hayarudi tena Kule yalikotoka. Yaani ni Kama haya makusanyo tunamkusanyia mtu. Matokeo yake karibu mikoa yote iko hoi kimiundombinu kiafya na kimaendeleo kwa watu wake kwa ujumla.
Kwa mfano Mkoa wa Dar kila sehemu ni mbovu, msimu wa Mvua ukiisha tu kila mwaka ni lazima barabara za Dar zianze kukarabatiwa upya, na hii siyo Dar peke yake, ni karibu mikoa yote. Tangu tupate uhuru kila Siku ni wimbo kwa Serikali kwamba wananchi wachangie ujenzi wa shule au vituo vya afya au madawati au nyumba za Waalimu, ili hali Serikali inakusanya kodi. That is unfear.

Kila mkoa ukiamua kukusanya kodi yake na kuitumia kwa maendeleo ya Mkoa husika, Nina Imani hii itapunguza matumizi mengi sana yasiyo na lazima. Hata Kama kila mkoa kila mwezi ukiitoa Gawio la 20% ya mapato yake, kwa Serikali kuu, bado mikoa itabaki na pesa nyingi ambazo zinaweza kuifanya hii mikoa ikapaa Zaidi Ulaya. Tunakwama wapi?

Chanzo: JamiiForums

No comments

Powered by Blogger.