MAAJABU YA NCHI YA ZAMBIA NA MALAWI

1. Nchi zote Malawi na Zambia zilipata uhuru mwaka 1964 na zote hutumia pesa aina ya Kwacha. Marais wake wote, Dk. Kamuzu Banda (Malawi) na Dk. Kenneth Kaunda (Zambia) walizitumikia nchi zao katika nafasi za urais kwa muda mrefu na asili zao zinatatanisha, hawaeleweki kama ni Wamalawi na Zambia. Wote Kamuzu na Kaunda walikuwa na kaulimbiu inayofanana ya “Wamuyaya” (Life) ikiwa na ishara ya mamlaka.


2. Bakili Muluzi, alizaliwa 1943, ndiye aliyechukua madaraka kutoka kwa Kamuzu Banda. Fredrick Chiluba, alizaliwa 1943, ndiye aliyechukua madaraka kutoka kwa Kenneth Kaunda, na wote wawili Muluzi na Chiluba walifanya jaribio la kutaka kubadili Katiba ili wapate kipindi cha tatu cha uongozi lakini walishindwa. Wote Muluzi na Chiluba waliwataliki wake zao kwa sababu ya kukosekana uaminifu kwenye ndoa.

3. Wote, Muluzi na Chiluba waliwapeleka watangulizi wao mahakamani (Dk. Banda na Dk. Kaunda).

4. Bakili Muluzi alimpendekeza Bingu wa Mutharika kuchukua nafasi yake, wakati Frederick Chiluba alimpendekeza Levy Mwanawasa kuchukua nafasi yake na wote waliwafanyia kampeni wakati wa uchaguzi.

5. Wote Mutharika na Mwanawasa walishinda uchaguzi na kuwa marais wa tatu katika nchi zao.
6. Muda mfupi baada ya kuchaguliwa kuwa marais, wote Mutharika na Mwanawasa walishindwa kuwabeba (kuwavumilia) watangulizi wao Muluzi na Chiluba. Wote wawili, Mutharika na Mwanawasa waliwapeleka watangulizi wao (Muluzi na Chiluba) mahakamani kwa makosa ya kujihusisha na rushwa. Sasa inavutia zaidi; Muluzi alishtakiwa na utawala wa Mutharika. Chiluba alishtakiwa na utawala wa Mwanawasa.

7. Bingu wa Mutharika alishinda kipindi cha pili cha uongozi, Mwanawasa alishinda kipindi cha pili cha uongozi. Mutharika alimchagua Joyce Banda kama Makamu wake wa Rais. Mwanawasa alimchagua Rupiah Banda kama Makamu wake wa Rais.

8. Mutharika alifariki akiwa madarakani katika kipindi chake cha pili kwa matatizo ya moyo (Cardiac Arrest). Mwanawasa pia alifariki akiwa madarakani katika kipindi chake cha pili kwa matatizo ya moyo (Cardiac Arrest).

9. Joyce Banda alichukua madaraka kutoka kwa Bingu wa Mutharika kutokana na kifo hicho. Rupiah Banda alichukua madaraka kutoka kwa Levy Mwanawasa kutokana na kifo hicho. Marais wote hawa waliochukua madaraka kutoka kwa marehemu waliitwa “Banda”.

10. Baada ya miaka 3, Rais Banda wa Zambia alishindwa kwenye uchaguzi na mpinzani wake Michael Sata. Banda wa Malawi naye ameshindwa kutetea kiti chake na mpinzani wake Peter Mutharika..!

No comments

Powered by Blogger.