MAGARI MAPYA YA WIZARA YA NISHATI KUTUMIA GESI BADALA YA MAFUTA

Waziri wa Nishati, Dk Medard Kalemani amesema magari mapya yatakayoanza yatakayolewa nchini kwa ajili ya wizara hiyo yatakuwa yameunganishwa na mfumo wa gesi ili kubana matumizi ya mafuta. 

Amesema lengo la uamuzi huo ni kubana matumizi ya mafuta, kutunza mazingira na kuhamanisha wizara nyingine na watu binafsi kutumia gesi. Wakati wizara ikichukua hatua hiyo, Aprili 2019 Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) lilianza mazungumzo na mradi wa mabasi yaendayo haraka (Dart) ili kuyawezesha mabasi ya mwendokasi kutumia nishati ya gesi. 

Ubungo baada ya kuunganishiwa mfumo huo na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Waziri huyo ametoa kauli hiyo jana Ijumaa Mei 31, 2019 Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya TPDC, ambayo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji), Angellah Kairuki. “Wizara tumeamua kuwa mfano kwa Serikali na Watanzania wote, tumekubaliana magari ya wizara katika idara zote tutakayoagiza katika awamu ijayo yatakuja yakiwa yameunganishwa na mfumo wa gesi.” 
“Hatuwezi kuhamasisha wengine tunaanza sisi kwa sababu ni gharama nafuu na inahifadhi mazingira, nitumie nafasi hii kuwaomba Watanzania kuanza kunufaika na gesi yetu ya hapa nchini,” amesema Kalemani.

Kalemani aliweka wazi nia hiyo alipokuwa akikagua gari linalotumia gesi badala ya mafuta baada ya kuuganishiwa mfumo huo kwa gharama ya Sh1.8milioni miezi sita iliyopita huku mmiliki wake, Linus Rugemalilra akieleza unafuu mkubwa katika kubana matumizi.

Kanuni za bei ya gesi asilia za mwaka 2016, zinaonyesha matumizi ya gesi hiyo katika magari husaidia kuokoa asilimia 40 ya gharama inayotumika katika ununuzi ya lita moja ya bei ya petroli na dizeli ya wakati husika. Hii ni sawa na kupunguza Sh40 katika Sh100 inayotumika katika mafuta ya kiwango hicho.

No comments

Powered by Blogger.