MUME APEWA TALAKA NA MKEWE. KISA?! ALIKUWA ANAMPENDA SANA

Mwanamke mmoja wa nchini Saudia amempa Talaka mumewe kupitia mahakama kwa sababu ya kupendwa sana na mumewe zaidi kuliko mama yake mume. Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 29 raia wa Saudia alipatwa na mshtuko mkubwa wa maisha yake kutoka kwa mkewe, baada ya kufikishwa mahakamani kwenye madai ya talaka. Mume alishanga sana na kutoelewa sababu ya mkewe kudai talaka, kwa sababu alikua anampenda sana mkewe na kumpa kila kitu anacho kitaka.

Mke alipo ulizwa na mahakama, alikiri kweli mume anapenda sana, na amekuwa akimpa kila anacho kitaka, pamoja na kupelekwa nchi mbalimbali duniani. Mke alisisitiza kuwa ni kweli anapendwa sana na mumewe zaidi ya mama yake mzazi mume. Na ili la kupendwa yeye sana kuliko mama mkwe (Mama wa mume) ndio linalomfanya aombe talaka.
"Siwezi kamwe kumwamini mwanamume ambaye anafanya kila kitu kwa mke wake lakini anakataa kumuhudumia mama yake," mwanamke huyo alimwambia hakimu. Mwanamke huyo alikiri kwamba mumewe umpa pesa nyingi, amesafiri nae safari nyingi za nje ya nchi na kumpa kila kitu alichotaka, lakini alisema hakutaka kuendelea na maisha yake pamoja naye. "Mtu asiye mzuri kwa mama yake mwenyewe hawezi kuaminiwa anaweza kunikataa hata mimi wakati wowote katika siku zijazo," alisema. Mume huyo alishangaa akamwuliza, "Je! Sijawacha familia yangu kwa ajili yako?"

Mke akajibu, "Ndio, na hii ndio sababu haswa ya kudai talaka kutoka kwako."

Mwanamke huyo alimwambia hakimu kuwa kila kitu ambacho mume wake alichokisema katika mahakama kilikuwa sahihi lakini alikuwa ameazimia kuachana nae kwa sababu alimpenda yeye zaidi ya familia yake, ikiwa ni pamoja na mama yake mzazi. Alimwambia hakimu kwamba hawezi kusubiri hadi siku ambayo mumewe atamuacha kama alivyo iwacha familia yake na ndugu zake. Mwanamke huyo alirudisha mahari na kuandikiwa talaka yake.

Mahakama ilimsifu mwanamke huyo kwa msimamo wake mzuri na hakimu akasema alikuwa na haki ya kuomba talaka, sababu ya mume kumpenda mwanamke zaidi ya mama yake mwenyewe ni ujinga. Alisema mkewe hakuwa na furaha kwa sababu alimfaidia zaidi kuliko mama (mume) aliyemzaa, akamlea na kutoa kila kitu maishani mwake kumlea na kisha kutothaminiwa na mtoto wake mwenye sababu ya mke.

Source: SaudiGazette

No comments

Powered by Blogger.