FAHAMU SIFA 15 ZA MNYAMA TWIGA

Kitu cha kwanza unachotakiwa kufahamu kuhusu twiga ni kwamba, hisia zake za kimapenzi zipo shingoni mwake! Sifa nyingine ni kama zifuatazo:

SIFA ZA TWIGA NI ZA KIPEKEE 

> Ni mnyama mrefu kuliko wote waishio ardhini na pia hupenda amani.

> Ni mnyama ambaye wanyama wenzake wanaokula majani hujisikia amani kukaa naye kwa kuwa huona hatari tangu ikiwa mbali, sasa usishangae wanyama kama pundamilia, swala wakijaa chini yake.

> Akikupiga teke na likakupata uwezekano wa kupona ni mdogo, hata wanyama wanaomuwinda huliepuka teke hilo, anapoinua mguu utaona hata simba akikimbia.

> Anatumia miguu ya mbele kama silaha yake wakati wa mapigano, nyuma hutumia inapibidi kama anapambana na mnyama zaidi ya mmoja ila ni nadra.

> Anahusudu kujitafuna, muda mwingi huutumia kwa kula.

> Ni mnyama mtalii anayependa kushangaa ulimwengu ulivyo, ndio maana hutumia muda wake wa ziada katika kutembea.

> Wakati wanyama wengine wakitumia muda mwingi kulala, pengine twiga ndio kiumbe pekee ambaye hulala muda mfupi kuliko viumbe wengine wote, hutumia saa mbili hadi nne tu, kama ana mtoto ndio yatakuwa pungufu ya hapo.

> Kiumbe huyu ana moyo mkubwa pengine ndio sababu wanavumilia mengi, moyo hufika hadi kilo kumi.

> Shingo yake ndio sehemu inayomsisimua kimahaba, wanapokutana dume na jike hufanya mchezo kama wa kuzungusha kwa kuzifunga shingo zao, mchezo huo humfanya dume kumpanda jike wake.

> Twiga jike ni maminifu kwa dume lake, jike naye hutafuta dume jingine endapo dume wake atakamatwa na wanyama wala nyama au kufa kwa ugonjwa na kama atakosa anaweza kufa kwa upweke.

> Wakati jike akiwa na sifa hizo kwa dume ni tofauti kidogo, lenyewe hupendelea majike wanaochipukia na wakati mwingine huweza kumpanda jike mwingine hata mbele ya jike wake.

> Binadamu anaweza kupita katikati ya miguu ya twiga kijana bila kugusa mwili wake, na bado ikabakia nafasi kubwa juu.

> Wanyama wanaowinda kama mnyama wanayemtafuta yupo jirani na twiga, huamua kubadili windo kwa kuwa twiga huharibu mbinu zao kwa sababu huwaona kwa urahisi.

> Mnyama huyu pamoja kwamba ni mpenzi wa amani, lakini usije ukamsogelea maana akikuhisi vibaya anaweza kukujeruhi kwa kurusha miguu yake, hivyo ni jambo jema kama utakuwa unamtazama kwa mbali kidogo na ukawa mtulivu kama alivyo  yeye.

Ni mnyama ambaye si mvivu na ana madaha pindi atembeapo.
Mnyama huyu anapatikana katika nyika hususan sehemu zenye migunga, ‘Vkwata’ pamoja na mikakaya,miti ambayo huifurahia sana kwani ndio ni chakula chake kikuu. Twiga hana ushindani mkubwa wa chakula na wanyama wengine kwa vile yeye hula majani ya juu nchani wakati wanyama wengine hawafikii majani hayo.

Twiga ana urefu wa kati ya mita 4.8 na 5.5 Uzito wake ni kati ya kilo 700 na 1500.Twiga jike ana rangi ng'avu zaidi kuliko dume.Hii inaweza kuwa ni maumbile ya kuwavutia Twiga dume.Dume ni mkubwa na mzito kuliko jike. Urefu wa ulimi wake ni kati ya sentimeta 46 hadi 50 wakati ambapo urefu wa moyo ni meta 0.6 Ana uwezo wa kukimbia kilometeta 55 kwa saa.Mkia wake ambao ni meta 2.4 ni mrefu kuliko mikia ya wanyama wote duniani.

UZAZI NA MZUNGUKO WA MAISHA.

Twiga hubeba mimba kwa siku 400 hadi 460 , ambazo ni sawa na miezi 14 hadi 15, ambapo mara nyingi huzaa ndama mmoja, huku mapacha ikitokea tu. 

Mama hujifungua akiwa amesimama na kondo lake hukatika mara moja mtoto aangukapo ardhini tofauti na wanyama wengine kama Ng’ombe ambapo huchukua saa kaqdhaa kondo kudondoka. Ndama akizaliwa huwa na urefu wa mita 1.8 na uzito wa kuanzia kilogramu 40 hadi 70 na Baada ya masaa kadhaa, mama huweza kukimbia japo ndani ya wiki mbili za mwanzo ndama hutumia muda mwingi kujilaza chini huku akilindwa na mama yake kutokana tishio la simba, chui, fisi au mbwa mwitu.

Wanayama hawa wanachangamoto kubwa katika maisha yao wawapo porini kwani ni asilimia 25 hadi 50 na maisha yao mara nyingi huishia kati ya miaka 20 hadi 25 kwa wale Twiga wa mwituni na miaka 28 wale wanaofugwa au kuishi nje ya mbuga.

No comments

Powered by Blogger.