MATOKEO YA KIDATO CHA SITA ACSEE 2019 YAMETANGAZWA
Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) nchini Tanzania leo Alhamisi Julai 11, 2019 limetangaza matokeo ya kidato cha sita ya mwaka 2019.
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa na Katibu Mtendaji wa Necta mjini Unguja Zanzibar, Dk Charles Msonde amesema ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 97.58 mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 98.32 mwaka 2019 ikiwa ni sawa na asilimia 0.74. Dk Msonde amesema mtihani huo uliofanyika kati ya Mei 6 hadi 23 mwaka 2019, watahiniwa 91,298 walisajiliwa wakiwamo wasichana 37,948 sawa na asilimia 41.56 na wavulana 53,350 sawa na asilimia 58.44.
Amesema kati ya watahiniwa waliosajiliwa, watahiniwa wa shule walikuwa 80,216 na watahiniwa wa kujitegemea walikuwa ni 11, 082. Katibu mtendaji huyo amesema kati ya watahiniwa 91,298 waliosajiliwa kufanya mtihani , watahiniwa 90,001 sawa na asilimia 98.58 walifanya mtihani na watahiniwa 1,297 sawa na asilimia 1.42 hawakufanya mtihani huo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za ugonjwa na utoro.
Dk Msonde amesema watahiniwa wa shule, kati ya watahiniwa 80,216 waliosajiliwa, watahiniwa 79,770 sawa na asilimia 99,44 walifanya mtihani ambapo wasichana walikuwa 33,883 sawa na asilimia 99.57 na wavulana 45,887 sawa asilimia 99.35. Watahiniwa 446 sawa na asilimia 0.56 hawakufanya mtihani. Amesema watahiniwa wa kujitegemea kati ya11,082 waliosajiliwa, 10,231 sawa na asilimia 92.32 walifanya mtihani na watahiniwa 851 sawa na asilimia 7.68 hawakufanya. “Jumla ya watahiniwa 88,069 sawa na asilimia 98.32 ya watahiniwa waliofanya mtihani wamefaulu,” amesema Msonde
Watahiniwa Kumi bora Kitaifa kwa masomo ya Sayansi kuanzia namba moja hadi kumi ni
1. Faith Nicholous Matee (St. Marry’s Mazinde Juu-PCB)
2. Herman Pauline Kamugisha (Kisimiri-PCM)
3. Levina Calist Chami (St. Marry Goretti-PCM)
4. Benius Eustace (Mzumbe-PCB)
5. Augostino Issaya Omari (Ilboru-PCB)
6. Satrumin Arbogast Shirima (Temeke-PCB)
7. Khalid Hussein Abdallah (Feza Boys-PCM)
8. Assad Y. Msangi (Feza Boys-PCM)
9. Peter Jovenal Riima (Kibaha-PCM)
10. Augustine J. Kamba (Feza Boys-PCM)
Wanafunzi 10 bora waliofanya vizuri kwa masomo ya Lugha na Sanaa ni
1. Victor G. Mtui (Feza Boys-EGM)
2. Paula Nelson Lujwangana (St. Marry’s Mazinde Juu-HKL)
3. Blandina Kessy Nyage (St.Marry’s Mazinde Juu-HGL)
4. Eva J. Shitindi (Machame Girls-HKL)
5. Ruhinda Benedicto Machimu (Geita Adventist-HKL)
6. Anita Zacharia Massawe (St.Marry Mazinde Juu-HKL)
7. Karimu Kassimu Muhibu (Nyangao-HKL)
8. Anold Andrea Msuya (Manyara-HKL)
9. Latifa Mohamed Mrosso (Ahmes-HKL)
10. Eliibariki Desidery Baliyanga (Lukole-HKL)
Waliofanya vizuri Kitaifa kwa masomo ya Biashara ni
1. Astone Stevin Ngaeje (Kibaha-ECA)
2. Gift M. Mwakikusi (Tusiime-ECA)
3. Emmanuel P. Chila (Alpha-ECA)
4. Athumani Magadula William (Umbwe-ECA)
5. Stephano Y. Dismas (Kibaha-ECA)
6. Robert John Tano (Scolastika-ECA)
7. Shabani H. Shabani (Kibaha-ECA)
8. Dotee A. Zuberi (Galonos-ECA)
9. Ernest P. Game (Kibaha-ECA)
10. Deogratias Ladislaus Msilinga (Kibaha-ECA)
Katika matokeo hayo Shule Kumi bora zilizoongoza Kitaifa ni
1. Kisimiri (Arusha)
2. Feza Boys (Dar es Salaam)
3. Ahmes (Pwani)
4. Mwandet (Arusha)
5. Tabora Boys (Tabora)
6. Kibaha (Pwani)
7. Feza Girls (Dar es Salaam)
8. St. Marry’s Mazinde Juu (Tanga)
9. Canossa (Dar es Salaam)
10. Kemebos (Kagera)
Shule Kumi zilizofanya vibaya Kitaifa ni
1. Nyamunga (Mara)
2. Haile Salassie (Mjini Magharibi)
3. Tumekuja (Mjini Magharibi)
4. Bumaangi (Mara)
5. Butuli (Mara)
6. Mpendae (Mjini Magharibi)
7. Eckernford (Tanga)
8. Msimbo (Katavi)
9. Mondo (Dodoma)
10. Kiembe Samaki A (Mjini Magharibi)
Leave a Comment