JE, BANDO LAKO LINAISHA HARAKA? SOMA HAPA KWANINI


Pengine si wewe mwenye matumizi mabaya na bando lako ila unajikuta unatumia bando kubwa zaidi kuliko matumizi yako madogo ya mtandao. Hili ni suala la kawaida kwenye simu za smartphone. Kuanzia sasa jua ya kwamba adui yako mkubwa wa bando lako la Data ni "DATA ROAMING".🤔
DATA ROAMING NI NINI..?
Data roaming ni mpangilio ambao unakuwezesha kutumia huduma za mitandao mingine ya internet hata bila ya kujisajili na mitandao hiyo,Kwa mfano "kama unatumia mtandao wa tigo kwa ajili ya matumizi ya data(mobile data) ni lazima utakua unapokea huduma za internet za kutoka tigo pekee. Lakini kwa kutumia mipangilio ya data roaming unaweza kutumia huduma za internet za vodacom kwenye laini yako ya tigo hata bila kua na laini ya vodacom kwenye simu yako. 

Data roaming imewekwa ili usiweze kukosa internet hata kama uko kwenye miji au nchi za ugenini pamoja na maeneo ya ndanindani(interior) ya vijijini. kama upo mahali ambapo mtandao wa internet haupo vizuri hasa vijijini basi Data roaming inakuhusu, kwa sababu kama unajua kabisa kwamba mtandao pekee wa kijiji fulani ni tigo na huduma yake ya internet inasumbua basi kwa kuwa wewe unatumia Vodacom au TTCL, kwa kuwasha Data roaming unaweza kutumia internet kwa speed nzuri kwa msaada wa mtandao wa tigoulioko eneo hilo.

ANGALIZO: DATA ROAMING NI GHARAMA, USITUMIE...!
Hili ndilo suluhisho pekee la matumizi mabaya ya bando lako la data kwani kuna gharama za ziada zinazohitajika ili kuwezesha huduma hii. Hakika hakuna kizuri kisicho na faida ðŸ˜ž kwa sababu pale ambapo unashindwa kutumia huduma ya internet unapokua sehemu mpya basi Data roaming itajaribu kutafuta mahali ulipo ili kuweza kukuunganisha na mtandao mwingine usiokuepo mahali apo. kinachofanyika ni kwamba taarifa zako zinatumwa kutoka kwenye mtandao huo unaosumbua kwenda kwenye mtandao wenye spidi nzuri ya internet. Taarifa zako zinapofika kwenye mtandao huo na kuonekana zinakidhi vigezo vyao ndipo unaporuhusiwa kutumia mtandao huo kwa wakati huo. Hivyo ni wazi kabisa ya kwamba mchakato huo unatumia gharama za ziada kwa sababu unahusisha makampuni mbalimbali tofauti ili kukuwezeshs wewe kupata huduma hiyo ipasavyo. Zipo njia nyingine nyingi za kitaalamu za uchambuzi wa gharama za Data roaming ambazao zinahitaji upeo mkubwa kuzielewa .

UTAJUAJE KAMA UNATUMIA DATA ROAMING...?
ni rahisi kugundua kama Data Roaming imewashwa. Kwani kwenye simu nyingi za Android na iPhone huonyesha herufi 'R' sehemu ya juu ya kioo cha simu yako, lakini kimuundo inaeweza kutofautiana kwenye baadhi ya simu. Kwa mfano unaweza kuiona alama kama hiyo kwa hapa chini(angalia mshale wa njano unapoelekeza).



HATUA ZA KUZIMA DATA ROAMING KWENYE SIMU YAKO 
Ukweli ni kwamba Data roaming ni nzuri sana katika kuongeza speed yako ya internet lakini pia ni chanzo cha data kumalizika kwenye simu yako pamoja na kupotea kwa senti kadhaa kwenye salio lako la kawaida. Unashauriwa kuizima sehemu ya Data roaming kama hauna matumizi nayo kwa kufuata hatua zifuatazo;

Kama unatumia simu za Android fanya hivi :
1. Ingia kwenye settings
2. Kisha Connnection
3. Halafu Mobile Networks
4. Baada ya hapo hakikisha sehemu ya data roaming imezimwa.

Kama unatumia simu za iPhone fanya hivi :
1. Ingia kwenye settings
2. Kisha mobile data
3. Halafu Mobile Data Options
4. Baada ya hapo hakikisha sehemu ya data roaming imezimwa.
KUMBUKA: Hatua hizo zinatumika pia pindi unapotaka kuwasha data roaming unapokua sehemu ambayo haina internet vizuri.
:kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na watoa huduma wa mtandao wa simu unaotumia.
:Unashauriwa kuzima sehemu ya data roaming endapo upo sehemu yenye uhakika wa internet.

HITIMISHO:
Zipo njia zingine nyingi zinazosababisha kupotea kwa bando lako la data na salio la kawaida ukiachana na Data roaming.  

Kwa mfano wa nyongeza usisahau kuzuia Apps kuji-update zenyewe kupitia playstore(Ni muhimu.....!). 

Fanya hivi kuzuia:
Ingia kwenye app ya playstore kisha fuata hatua hizi setting>Auto-update apps>Don't auto-update apps>Done, mpaka hapo utakua umemaliza kuzuia tatizo la simu yako kuji-update kila wakati bila ya wewe kuiamuru kufanya hivyo na utakua umezuia tatizo la kupotea kwa data kiholela holela.

Chanzo: JamiiForums

No comments

Powered by Blogger.