MWANAJESHI ALIYEOKOTA PESA NA KUZIRUDISHA, ALIPWA MARA MBILI NA KUPANDISHWA CHEO KWA NGAZI MBILI
Afisa wa Jeshi la Anga la Nigeria, ACM Bashir Umar aliyerejesha mkoba aliouokota wakati akiwa kazini uliokuwa fedha sawa na Tsh. Milioni 95.2 milioni amepandishwa cheo kwa ngazo mbili.
Kufuatia hatua hiyo, sasa Umar anakuwa ni Koplo. Kwa kufuata taratibu za kawaida, ingemchukua Umar takribani miaka 10 kufikia ngazi hiyo. Mkuu wa jeshi hilo, Saddique Abubakar alimsifu kwa uaminifu wake, na kwamba kitendo chake kimelijengea jeshi hilo jina zuri miongoni mwa wananchi.
Leave a Comment