OPERA HOUSE HEIST: UHALIFU ULIOKAMILIKA

Kuna wakati unaweza kujiuliza wezi wamewaza nini, kisha kuja na mpango flani wa uvamizi. Kwa sababu mtu anapanga tukio la wizi mpaka unabaki kujiuliza huyu ni binadamu mwenzetu kweli au ametoka sayari nyingine? Hili ni kutokana na akili kubwa iliyotumika katika upangaji wa matukio mpaka wizi wenyewe! Na ndicho kilichotokea kwenye wizi huu.


Opera house ni jengo kubwa la kifahari huko jijini Mumbai nchini India, ambapo ndani yake kuna duka la kuuzia vito vya thamani kama mikufu, bangili, pete, madini n.k. ndani ya jengo kwenye duka hilo ndiko kulikofanyika wizi wa akili kubwa ambao ulishangaza dunia nzima na kubaki kuwa moja ya wizi uliotumia ustadi wa hali ya juu kabisa, nah ii ni kuanzia mipango hadi kuvamia ndani ya Opera house.

Wizi huu haukuhitaji washirika wa kupanga namna ya kuvamia na kuiba, kwani mpangaji wa wizi huu hakuwa na haja ya kufanya hivyo ila akaamua kufanya peke yake na bila kutumia silaha ya aina yoyote ile. Mkurugenzi mtendaji mstaafu wa Central Bureau of Investigation (CBI) Bw. M.G. Katre alifanyiwa mahojiano na gazeti maarufu sana nchini India lijulikanalo kama The Times of India, kwani Katre alikuwa madarakani kipindi wizi uo unatokea na lihudumu kwa takribani miaka mine (Februari 28, 1985 mpaka Octoba 31, 1989) na alipoulizwa kuhusu wizi huo alijibu kwa ufupi tu “perfect crime”maanake uhalifu uliokamilika.

Twende kwenye tukio lenyewe…..


Mnamo Machi 19, 1987 mchana wake Kamanda wa polisi Idara ya uhalifu Bw. Arvind Inamdar alipokea simu ya uharaka akiwa katika ofisi yake Jijini Mumbai ambapo ndipo makao makuu ya polisi. Simu hiyo ilipigwa na tycoon mmoja itwaye Pratapbhai Zevari ambapo alikuwa akimiliki duka kubwa la vito vya thamani lijulikanalo kama Tribhovandas Bhimji Zhaveri (TBZ), kuwa mbona kiongozi wa CBI amekuja na kuacha vijana hapa na ni nusu saa tangia aondoke simu ikakatika kwa bahati mbaya na akapiga tena muda huo huo na kuendelea na maongezi.


Turudi nyuma kujua kwanini simu hiyo ilipigwa kwa Inamdar? Terehe 15 Machi 1987, jamaa mmmoja kwa muonekano alikuwa mhindi mwekundu, mrefu kidogo kwa kimo na umri kati ya miaka 45 hadi 55, jamaa huyo alikuwa amevalia suti nyeusi ya kung’aa na briefcase mkononi ya rangi ya kahawia. Huyo jamaa alifika katika hoteli moja jijini Mumbai iitwayo Taj Intercontinental, ni moja ya hoteli ya kifahari jijini humo kwani ina hadhi ya nyota 5 na kimuonekano alikuwa anaendana na hadhi ya hoteli hiyo.

Huyo jamaa alipofika hotelini hapo alienda moja kwa moja mpaka mapokezi na kukutana na dada aliekuwa kwenye deski la mapokezi na kuanza kuzungumza naye kwa kumuambia anataka chumba hotelini hapo kwa siku nne yaani Machi 15 mpaka Machi 19, akamjibu kuwa chumba kipo na kilikuwa kimebaki kimoja tu. Chumba kilibaki kimoja kwa sababu jijini hapo kulikuwa na mkutano wa kimataifa na ulihudhuriwa na viongozi wengi wakubwa ambapo sasa booking ya vyumba ilikuwa kubwa sana na kupelekea uhaba wa vyumba, jamaa huyo akaambiwa chumba ambacho kipo wazi ni chumba namba 415. Akajitambulisha kwa majina Mohan Singh na anatokea himaya ya Kerala katika mji mkuu wake wa Trivandrum.

Baada ya kukamilisha taratibu zote zinazohitajika katika hoteli hiyo Singh alisindikizwa na mhudumu wa hoteli na kufikishwa moja kwa moja kwenye chumba chake namba 415. Jamaa huyo kimuonekano alifanania kama mwanausalama na ukizangatia kulikuwa na viongozi wakubwa jijini hapo kwa hiyo lazima wanausalama kuwa wengi maeneo mbali mbali jijini hapo hasa hapo hotelini kwa usalama zaidi. Singh kesho yake yaani tarehe 16 Machi 1987, asubuhi alielekea kwenye gazeti kongwe la nchini humo la The Times of India akiwa na ombi la kutaka kuweka tangazo katika gazeti lao, ambalo alitaka litokee kesho yake yaani tarehe 17 Machi, msimamizi wa kitengo cha matangazo na biashara cha gazeti akampa mchanganuo mzima wa gharama za kuchapisha matangazo jamaa akalipia kiasi kilichohitajika na akaelekea kwa mhariri wa matangazo na kumuelezea namna tangazo lake anataka litokee katika gazeti hilo.

Kesho yake gazeti lilivyotoka kulikuwa na tangazo la Bw. Singh, ambapo tangazo hilo lilikuwa linahusuiana na masuala ya ajira na lilikuwa na maneno haya “Kunahitajika wahitimu wa ngazi ya chuo katika nafasi za maafisa wa intelejensia na maafisa ngazi za ulinzi na wanahitajika kuripoti katika hoteli ya Taj Intercontinental tarehe 17 Machi 1987, saa nne kamili asubuhi''. Basi kesho yake lile tangazo likatokea kwenye gazeti hilo na ikumbukwe kwa miaka hiyo watu walikuwa wanayategemea sana magezeti kama chanzo kikuu cha habari tofauti na miaka hii ambapo teknolojia imekua kwa kasi na kuwa njia kadha wa kadha za mawasiliano.

Kesho yake tarehe 18 Machi, muda wa saa nne asubuhi nje ya hoteli ya Taj walijitokeza watu wengi waliokadiriwa kufikia 46 wakimsubiri mhusika wao maana walikuwa na kiu ya ajira hiyo iliyotangazwa na kila mmoja akiwa amejipanga kwa usaili wa siku hiyo. Singh alitoka nje ya hoteli hiyo na kukutana na watu hao ambapo wengi wao walikuwa vijana watafutaji na kuwaambia hawatoweza kufanyia usahili hotelini hapo kama iliyokuwa inajulikana na ni kutokana na sababu za kiusalama zaidi. Kwani hotelini hapo kulikuwa na viongozi wengi wakubwa na tutaelekea “Mital Tower”kwa ajili ya kuendelea na usahili wetu alisema Singh.

Jana yake aliporudi kutoka katika mizunguko yake alitaarifiwa ya kuwa ombi lake la kufanya usahili hotelini hapo halitawezekana tena kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao, ila menejaalionekana kuwa na wasiwasi wa kiusalama kwa wageni hao waliofika hotelini hapo kwa ajili ya mkutano huo wa kimataifa. Baada ya Singh kupata hizo taaarifa akaamua kutafuta mbadala haraka sana, na jana yake ya tarehe 17 Machi ndipo alipofanikiwa kupata ukumbi wa kufanyia usahili huo huko Narman katika mji wa kibiashara jijini Mumbai kwa kukodi ukumbi hapo Mital tower kwa ajili ya kesho yake.
Basi wakaelekea wote huko na usahili ukaanza mara moja kwa waombaji hao tena alikuwa mwenyewe bila msaidizi yeyote yule. Alifanikiwa kuwafanyia wote usahili siku ile ile na kufanya mchujo mwenyewe kulingana na vigezo alivyovitaka na alifanikiwa kupata vijana takribani 26 kati ya 46, akawashukuru hao 20 waliokosa nafasi kwa ushiriki wao. Singh wakati wa usahili alijitambulisha kuwa ni nani na ametokea shirika gani kwani kwenye tangazo lake hakuweka wasifu wake. Akajinasibu ya kuwa ni ofisa wa juu CBI na watakaofanya vizuri atawaajiri kwenye shirika hilo na kuwa mmoja wa maafisa kwenye shirika hilo, kwa maneno mengine waomba kazi walipagawa kweli kweli kwa kuona wameulamba endapo wangepata nafasi kwa kushinda usahili huo na ni kutokana na sifa za CBI.

Wale 26 walioshinda waliambiwa waache nakala na picha ili aweze kuwatengenezea vitambulisho vya muda kwa kazi inayofuata kesho yake, wakafanya hivyo na Singh akawapa kiasi fani cha hela kwa ajili ya nauli. Akili ya kazi aliyotumia Singh ni kuwaambia kesho yake mchujo unaendelea hivyo kutakuwa na majaribio ya vitendo, yote hii ni kuzidi kuwapa morali waombaji wa kazi kabla ya kuondoka akawaambia muongozo wa majaribio hayo atawapa kesho yake hapo hapo walipofanyia usahili na aliwasihi kuzingatia muda.

Basi akaagana nao, nay eye akarudi hotelini kwake na kuanza mara moja kuwatengenezea vitambulisho vya muda kama maofisa wa CBI na yote ni kwa ajili ya kazi ya kesho yake. Hii CBI ni kama ilivyo FBI ya nchi Marekani kiutendaji kazi. Kesho yake asubuhi na mapema wale vijana 26 wakawa wameshawasili eneo lile kwa ajili ya kuendelea na hatua inayofuata, wakamkuta Singh ameshawasili na anawasubiria na mara moja akaanza kuwapa maelekezo nini wanatakiwa kufanya. Akaanza kwa kuwaambia tunaanza kwa kwenda duka kubwa la TBZ ndani ya Opera house, sisi kama CBI tumepata taarifa mbaya kuhusu duka hilo kwamba kuna uuzwaji wa bidhaa bandia pia kuna ukwepaji wa kodi na ndicho kilichonilazimu kuunda timu ya siri na kutaka nguvu mpya kwani najaua itakuwa na ari ikilinganishwa na maofisa wangu wengine ambao washazoea ofisi na wataangiwa na tamaa ya pesa na kuhadaiwa na rushwa hivyo kuitoifanya hii kazi kwa umakini.

Na kuendelea kuwaambia, jana kuna kitu sikuwadokeza kuwa kuna timu kama hii sehemu nyingine nayo inafanya ukaguzi ila wapo na kiongozi mwingine, nako nitaenda kuona kazi inaendeleaje, kundi litakalofanya vizuri ndilo litakalopata mkataba wa kufanya kazi na CBI na mimi ndiye nitaketoa alama kwenye ufanisi wenu. Akaendelea kuwambia tukifika pale, tutaingia kwa kuvamia kwani tukiwapa taarifa mapema wataficha vitu hivyo bandia hata vitabu vya mahesabu wataficha hivyo mnatakiwa kuweka hofu pembeni na kuwa majasiri kwani tunafanya kazi ya kiserekali kwa mamlaka ya taifa la India.

Baada ya maelezo hayo Singh akapigia simu basi moja zuri ambalo teyari alikuwa amelikodi kwa ajili ya kuelekea Opera house. Basi likafika na kuingia wote na Singh mwenyewe na safari ikaanza kuelekea TBZ. Walifika Opera house saa 8:15 mchana, Singh akaanza kushuka na kuelekea TBZ moja kwa moja, ndani aliwakuta wahusika ambao ni wauzaji katika duka hilo na akajitambulisha kuwa ni ofisa wa CBI na akawaonesha kitambulisho chake. Baada tu ya kujitambulisha akaomba kuonana na bosi wao kwa kudai ana maongezi naye, basi mfanyakazi mmoja akamsindikiza yule jamaa mpaka kwenye ofisi ya bosi wao na kumwambi kuna ofisa kutoka CBI anamuulizia na Zevari bila hiyana akamruhusu aingie ndani.

Wakasalimiana na Singh akajitambulisha tena kuwa ni ofisa wa CBI na akaonesha ID yake. Basi akendelea kumwambia wamepata taarifa kutoka msamaria mwema ya kuwa duka lao linauza vitu bandia na lina ukwepaji wa kodi kwa kudanganya mapato yao ya kila mwezi na hivyo anakiuka sharia za nchi, hivyo yeye na timu yake wamefika dukani hapo kukagua mali hizo na vitabu vya fedha kuona ni vipi wanakwepa kodi na wakibaini hilo watamchukulia hatua za kisheria. Zevari akaanza kuingiwa na wasiwasi japokuwa alijua hana vitu bandia dukani mwake ila tu ugeni huo wa CBI ulimtisha kwani hajawahi kutembelewa ama tu kukaguliwa na maofisa wake.

Singh kuthibitisha yupo kazini akamuonesha kibali cha upekuzi (search warrant) kuwa yeye na maofisa wake 26 wapo hapo kukagua vito vyake na hivyo vitabu vya fedha kuona ukwepaji kodi wa huyo tycoon. Basi Zevari hakusita kuwaruhusu kufanya ukaguzi wao, kwani CBI wapo kihalali na kisheria kufanya kazi hiyo, Singh akaelekea moja kwa moja kwenye basin a kuwaelekeza vijana wale kuingia ndani moja kwa moja kwenye hilo duka na walipoingia tu wakakutana na Zevari ameshatoka ofisini na Singh akamtambulisha kwa hao vijana wake ya kuwa na maofisa wa CBI na atasaidiana nao kwenye ukaguzi huo hapo dukani kwake.

Akaruhusiwa kuanza kazi , ila kabla ya yote akawaambia kwa mujibu wa taratibu zao za kiutendaji lazima kamera zote zizimwe na kusiwe na muingiliano wa watu dukani hapo yaani kuingia na kutoka kwani italeta usumbufu na mkanganyiko katika utendaji wa kazi yetu, kusiwe na simu ya aina yoyote ile kupiga ama kupokea wakati ukaguzi unaendelea kiufupi kusiwe na movement za aina yoyote ile ndani ya duka hilo ili kuepusha janja yoyote kutokea kwenye zoezi lao na mwisho akaomba leseni ya silaha zao za ulinzi kukagua kama ni halali pia. Basi waliitikia wito wake na kamera zikazimwa na wakaweka ishara ya kuwa duka duka hilo limefungwa ili kuondoa msongamano, pia wakamkabidhi leseni alizoomba na kazi ya ukaguzi ikaanza mara moja.

Singh akawaelekeza vijana wake wamkabidhi vito kwa ajili ya yeye kuvikagua ubora na wengine wapiti vitau vya fedha kuangalia sehemu zinazoonesha kuna ukwepaji wa kodi ikilinganishwa na mauzo yake. Wakati zoezi likiendelea Singh aliwaagiza vijana wake kuweka vito vya thamani kwenye briefcase yake na kiasi flani cha hela, baada ya kama dakika 45 za ukaguzi Singh aliagiza vijana wake wawili kuipeleka briefcase hiyo kwenye lile basi walilokuja nalo huku yeye akiendelea na ukaguzi, wakaitikia wito wakavipeleka na kurudi navyo ndani.

Dakika kumi baadaye Singh akawaambia kuwa anaendelea na ukaguzi sehemu nyingine na anawaacha vijana wake hapo, Zevari kabla ya kumruhusu Singh kuondoka akamuuliza kati ya makossa hayo amwili niliyoshutumiwa nayo umeona lolote lile? Akamjibu nitakaporudi kutoka kwenye ukaguzi wa duka jingine nitakupa ripoti ya awali ya ukaguzi na ninawaacha vijana wangu hapa wamalizie ukaguzi.

Ikapita saa moja bila mrejesho wowote ule, ikabidi Zaveri awaulize wale vijana mbona kiongozi wenu hajarudi mpaka sasa huku kazi zangu zimesimama, vijana wakamjibu kuwa wanachojua kiongozi wao kaenda kufanya ukaguzi duka jingine ila hawafahamu ni wapi! Taa nyekundu ikawawaka kichwani mwa Zaveri na akahisi kuna mchezo mchafu na ikabidi sasa apige simu polisi na kuwasiliana na kamanda Inamdar kama nilivyoeleza hapo mwanzoni na simu ikakatika.

Na sasa tuangalie waliongea nini alipopiga simu mara ya pili……

Zaveri alimwambia kuna afisa wa CBI alikuja hapa mchana na aliondoka na baadhi ya vito na hela, huku akiwaacha vijana wake hapa wapo 26 na kufanya shughuli zangu zisimame. Kamanda akashtushwa na tarifa hizo, kwani hana taarifa za CBI kufanya ukaguzi katika eneo lake hilo la kipolisi, ila hakuonesha mshangao huo kwa Zaveri kwani CBI kutokana na unyeti wa baadhi ya kaguzi wanaweza wasitoe taarifa polisi, hivyo akamwambia ngoja awasiliane na CBI nione inakuwaje halafu nitakurudia.

Akawasiliana na makao makuu CBI na kuwapa taarifa hizo, nao wakashangaa na kumjibu mbona hawana ukaguzi kwenye jiji hilo? Kusikia hivyo kamanda akajihakikishia ya kuwa wale si CBI, akamrudia Zaveri na kumuuliza hao maafisa bado wapo? Akamjibu ndiyo ila kiongozi wao hayupo, akaona ndio mwanga wa kuwatia nguvuni vijana hao, basi akaongozana na askari wengine kuelekea dukani hapo na mara moja akawaweka vijana hao chini ya ulinzi.

Vijana wale wakawa wabishi, kwamba inakuwaje wanawekwa chini ya ulinzi wakati wanafanya kazi ya kiserekali, wakati mabishano yakiendelea maafisa wa CBI wakafika eneo la tukio na kuanza kukagua vitambulisho vyao na wakagundua kweli vinafanana na vya kwao ila ni bandia. Hapo sasa ndio wale vijana wakagundua wameingizwa mkenge na Singh. Kabla ya kuondoka nao wakaanza kuchukua maelezo ya awali kumuhusu boss wao ili waweze kufanya uchunguzi kamili...

Itaendelea...

No comments

Powered by Blogger.