OPERA HOUSE HEIST: UHALIFU ULIOKAMILIKA (Sehemu ya 2)

Maafisa wa CBI baada ya kupata maelezo ya awali wakaanza kulifuatilia lile basi lilowaleta pale, kuwa lilotekea wapi na hivyo wakaenda moja kwa moja katika ile hoteli aliyofikia Singh na kuchukua maelezo kutoka kwenye ile hoteli kutoka kwa yule dada wa mapokezi aliyempokea awali. Kutokana na yale maelezo waliyoyapata maafisa wa CBI, lile basi lililowapeleka wale maafisa bandia na Singh mwenyewe ni mali ya ile hoteli, ikimaanisha lilikodiwa kutoka katika magari ya hoteli kwa ajili ya wateja wao na hivyo wale maafisa wakaomba wafanye mahojiano na dereva wa hilo basi kwani yeye ndio mtu wa mwisho aliyeondoka na mtuhumiwa huyo.



Meneja wa hoteli naye alikuepo akisikiliza hayo mazungumzo kati ya dada wa mapokezi na maafisa wa CBI, kwa hiyo meneja kuona kunahitajika yule dereva wa basi lilowapeleka wale maafisa feki alimuita mara moja kwani alikuwa amesharudi muda mrefu hotelini hapo baada ya kumaliza kuwapeleka walikomkodi.
Dereva alifika pale hotelini na kuanza kuhojiwa na maafisa wa CBI kuwa yule jamaa walienda nae mpaka wapi? Dereva alianza kueleza kuwa alimuamuru aondoke bila wale vijana wengine tuliokuja nao na kuniambia tuelekee mitaa ya katikati ya jiji na kushuka sehemu ya kituo cha taxi kwenye eneo la Vila Parle na kuniambia nisirudi tena kule Opera house, kwani wale vijana nishawaelekeza waondoke zao kuelekea majumbani mwao baada ya kutoka pale.

Maafisa wa CBI wakamuuliza vipi kuhusu briefcase za vitu alivyowatuma wale vijana wawili walete kwenye gari navyo vipo wapi? Akawajibu kuwa yule jamaa alishuka navyo pale stand ya taksi na hakuacha kitu chochote ndani ya basi. Ikabidi maafisa wa CBI wajigawe kwa makundi kwenda moja moja kwenye hicho kituo cha taxi na kundi jingine likabaki pale hotelini kwenda kufanya upekuzi na uchunfuzi ndani ya chumba no. 415 ambacho ndicho alichofikia na alikuwa hajakiachia, kuona kama kama watakuta chochote kimesalia ili kiweze kuwasaidia kwenye chunguzi zao.

Wale walioenda kwenye kituo ch taxi walianza mahojiano na madereva wa taxi wa kile kituo, kwa bahati nzuri madereva wale waliwapa ushirikiano mkubwa sana maafisa hao kwa kuwaeleza ni kweli kuna mtu kama huyo alichukua taxi hapa na dereva aliempeleka alikuwepo pale. Kwa hivyo maafisa wakamgeukia yeye kwa ajili ya mahojiano.

Dereva yule akasema alimpeleka mpaka maeneo ya karibu na nje ya mji na kumshusha hapo na jamaa akachukua gari iliyokuwa imepakiwa pembeni na kuondoka zake, yeye hakuhisi chochote hivyo hakumfuatilia kuwa alienda wapi. Dereva akawaelekeza eneo alilomshushia yule jamaa, na maafisa wakaelekea huko mara moja kuona kama watafanikiwa kupata taarifa yoyote.
Mafiasa walifika mpaka pale aliposhushiwa yule jamaa na kuanza kuhoji watu wa maeneo yale waliokuepo wakati jamaa anashuka kwenye taxi na kupanda gari jingine, na mashuhuda hawakuwa na taarifa za kutosha kumhusu huyo jamaa kwani hawamfahamu na hawakumtilia maanani kuwa atakuwa ni mtuhumiwa wa wizi. Kwa hali hii maafisa wa CBI wakawa hawana taarifa zilizojitosheleza za kumfuatilia huyo jamaa kuwa atakuwa ameelekea wapi!

Nao wale maofisa waliobaki hotelini hawakuambulia chochote kule kwenye kile chumba cha jamaa alichofikia, ikabidi warudi kituoni na kukuta wale wengine wanaendelea na mahojiano na wale maafisa bandia 26 na kukuta wenzao wamegundua kuwa hao vijana walitumika katika mpango wa wizi bila kujijua! Na wengi walikuwa wafanyakazi wa serikali ila walikuja kugombania nafasi mpya zilizotangazwa ili kuongeza maslahi. Hata hao maafisa feki hawakuwa na taarifa za kutosha kuhusu huyo jamaa aliewafanyia usahili.
Wale vijana walilala pale kituoni mpaka kesho yake kwa ajili ya kumalizia mahojiano na CBI ili wajidhihirishe kabisa kuwa hawahusiki na mpango mzima wa tukio. Kesho yake waliweza kuwaachia mchana wake vijana wote baada ya kuona hawana hatia ila tu ni kiuu ya maslahi mazuri ndiyo iliyowapelekea kuingia kwenye mtego mtego uliotaka kuwapeleka kwenye matatizo makubwa.

Maafisa walienda pia kwenye ofisi za gazeti la The Times of India kwa ajili ya mahojiano kuona kama watapata taarifa za kutosha kuhusu huyo jamaa maana aliweka tangazo lake la kazi kwenye gazeti lao, maelezo waliyoyapata pale hayakuwa na msaada wowote ule kwasababu hayakuwapa mwanga wowote ule kuhusu huyo jamaa ni nani.

Kulikuwa na doria katika jiji zima la Mumbai katika vituo vya mabasi, viwanja vya ndege na mipaka yote ya jiji kuona kama wanaweza kubaini kama atakuwa bado hajaondoka katika jiji hilo na hawakufanikiwa kwa chochote. Maelezo waliyoyachukua pale hotelini ni pamoja na jina la jamaa alilojiandikiasha na sehemu aliyotokea, hivyo kufanya timu kuundwa na maafisa wa CBI kwenda kwenye himaya ya Kerala ili kumtafuta huyo jamaa jamaa kama wanaweza kumpata ingawa walijua siyo rahisi kumpata kwa mtu mwenye akili hivyo kupanga tukio kama hilo ataje kweli sehemu aliyotokea! Ila timu ilienda kule ili kujiridhisha kwani kuna makosa mwizi anaweza kuyafanya na usitegemee.

Timu ilenda Kerala na kufika salama na kuaza uchunguzi kwa kuwela kambi katika himya ile kwa muda mrefu ila hakuambulia chochote katika uchunguzi wao mzima. Na mpaka kufikia hapo taasisi ya CBI ilikuwa imeshapangwa kwa kuonekana Dhahiri kuwa wameshindwa kumpata jamaa au hata vidokezo ambavyo vina mwanga kuweza kumng’amua huyo jamaa, ingawa hawakukubali kushindwa na kuendelea na chunguzi zao.

Baada za juhudi CBI kule Kerala kuonekana hazizai matunda, na kuwapelekea kumuweka huyo jamaa kwenye kundi la “The Most Wanted” duniani na hili ni kutokana na muda kwenda na hakuna dalili za kumtia nguvuni. Kwa mantiki hii sasa wakaihusisha dunia nzima, na kuamua kushirikisha pande mbali mbali duniani na kuanza kutoa tahadhari kwa taasisi nyingine za masuala ya upelelezi katika nchi nyingine duniani kuhusu huyo jamaa na kutoa taarifa zake za awali pamoja na taswira yake.

Taasisi nyingine za kiupelelezi huwa zinatoa ushirikiano hasa kwa muhalifu aliyeonekana kusumbua vichwa vyao na ndicho kilichotokea kwa jamaa huyo kuona kama kama atakuwa amekuja kujificha katika nchi zao. Baada ya muda mrefu kukaja kupatikana taarifa kuwa kuna mtu aliedhananiwa kuwa ndio Singh aliyefanya uhalifu ndani ya Opera house nchini India. Mara moja baada ya CBI kupata hizo taarifa wakaemda kumkamata huyo jamaa aliyejulikana kama George Augustine Fernandes na kumsafirisha mpaka Mumbai kwa ajili ya mahojiano.

Baada ya mahojiano na uchunguzi wa muda mrefu wakaja kubaini kuwa huyo jamaa hakuhusika na tukio hilo, na kilichomgharimu huyo jamaa kuhusishwa na uhalifu huo ni kutokana na tabia yake ya kuiba sana vitu na siku ya tukio lilivyotokea hakuwa katika mji wake na mwishoni akaonekana si yeye.
Miaka ikazidi kusonga na mhalifu wao hajapatikana, na kuwafanya CBI waonekane kama wamemshindwa Singh na katika nchi nyingine nako hawakuweza kumpata na hakuwa na taarifa zozote kama yupo katika nchi zao.

Mnamo mwaka 1990 zilikuja taarifa kuwa Singh ameonekana Dubai anakula bata na kufanya CBI kuunda kikosi kazi mara moja kuelekea huko kwa ajili ya kumsaka na kumkamata. Timu ilisafiri mpaka Dubai kwa kazi ya kumsaka na kumkamata huyo jamaa na kusaidiana na wanausalama wa Dubai katika kuhakikisha wanamtia nguvuni Singh katika kuhakikisha wanamtia nguvuni Singh asijegundua kuwa wao kama CBI wamefika teyari Dubai kwa ajili ya kumtafuta na kumkamata.

Timu iliyoenda Dubai ilka zaidi ya mwaka na nusu ila hawakufanikiwa kumpata, na mkurugenzi wa CBI aliamua hiyo timu irudi tu nchini India kwani hakuna dalili za huyo jamaa kuwepo Dubai na kama alikuwepo basi alishashtuka uwepo wa CBI na kumfanya atoroke. Mpaka kufikia hapa kesi hii ilishakuwa ngumu kwa CBI ingawa hawakukiri hadharani kushindwa kumaoata huyu jamaa ila dunia ilishajua kuwa wamegonga mwamba na kushindwa kumng’amua huyo Singh ni nani na yupo upande gani wa dunia hii..!!

No comments

Powered by Blogger.