ALIYEKUWA RAIS WA ZIMBABWE, ROBERT MUGABE AFARIKI DUNIA

Bwana Robert Mugabe amefariki dunia huko Singapore baada ya kuugua kwa muda mrefu! Taarifa hii ni kwa mujibu wa Waziri wa Elimu wa Zimbabwe. Amefariki akiwa na miaka 95!


Gazeti la Mwananchi limeandika:

Dar es Salaam. Aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zimbabwe na mpigania uhuru wa nchi hiyo, Rober Mugabe amefariki dunia. Kwa mujibu wa familia ya Robert Mugabe, imeeleza kiongozi huyo amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu. Rais Mugabe ambaye alipigania uhuru wa nchi hiyo hadi lilipopata uhuru Aprili 18, mwaka 1980, aliliongoza taifa hilo kwa miongo mitatu kuanzia mwaka huo hadi alipoondolewa madarakani kwa njia ya mapinduzi ya kijeshi Nov 2017. 
Waziri wa Elimu wa Zimbabwe, Fadzayi Mahere ametoa taarifa ya kifo cha Mugabe kupitia ukurasa wake wa Twitter akiandika “Pumzika kwa amani Robert Mugabe.” Rais Mugabe alizaliwa Februari 21, mwaka 1924 katika nchi hiyo wakati huo ikiitwa Rhodesia. Robert Mugabe pia aliwahi kufungwa jela kwa zaidi ya muongo mmoja bila kufunguliwa kesi baada ya kuikosoa Serikali ya Rhodesia mwaka 1964.

No comments

Powered by Blogger.