MATOKEO YA DARASA LA SABA 2019

Baraza la mitihani Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2019 ambapo asilimia 81.50 ya watahiniwa 933,369 wamefaulu mtihani huo huku watahiniwa 909 wakifutiwa matokeo kwa sababu ya udanganyifu.
Aidha katika matokeo hayo, Grace Imori Manga wa shule ya msingi Graiyaka ya mkoani Mara ametangazwa kuwa wa kwanza kitaifa akifuatiwa na Francis Gwaniwa shule y msingi Paradiseya mkoani Geita huku namba tatu ikishikiliwa na Lio Kitundu wa shule ya msingi Mbezi ya Dar es salaam.

No comments

Powered by Blogger.