Kwa wapenzi wa muziki wa Hiphop nchini Tanzania bila shaka jina 'Andre K' sio geni kwao. Ni msanii wa hiphop aliyekuwa akiwakilisha kundi la Dom Down Click (DDC). Andre K anafahamika kwa nyimbo zake nyingi kama Gangster Still Alive (G.S.A), I Wish ft. Miracle, Nenda kasome ft Slimsal, Karibu Chuo, Kachetuka ft Adam Shule Kongwe, Bora Usingeenda Shule (Elimu ya juu) ambayo ni jina la EP ya Andre K ambayo ilitoka mwaka 2017.
Andre K amefariki leo (jana) baada ya kuanguka bafuni na akapelekwa hospitali ya Benjamin Mkapa ambapo mauti yalimkuta huko. BlackMutu Blog inatoa pole kwa wote walioguswa na msiba huu wa msanii Andre K, bwana alitoa bwana ametwaa. Mungu amlaze mahali pema peponi. Amen!!
Leave a Comment