PIC OF THE BLOG: AMBWENE YESSAYA "AY" AND YOUNG GURU

Wengi wanaweza kuwa hawamfahamu huyu jamaa. Anaitwa Young Guru, ni DJ na sound engineer rasmi wa Jay Z na anatajwa kuwa engineer aliyefanikiwa na kuheshimika zaidi kwenye historia ya Hip Hop.
Kama umeiona Fade to Black, utakuwa umemuona sana humo akirekodi sauti za Jay Z studio.
Pamoja na kuhusika sana na kazi za Jay Z, Young Guru pia amefanya kazi na wasanii wengi wakubwa wakiwemo Beyonce, Rihanna , Ludacris, Ghostface Killah, Freeway, Cam'ron, Redman & Method Man, Mariah Carey, Pete Rock, Fabolous, Talib Kweli, Bone Thugs-N-Harmony, T.I, Mary J Blige na wengine.
Alikuja Tanzania wiki iliyopita na ilikuwa ni heshima kubadilishana naye mawili matatu.

No comments

Powered by Blogger.