TAZAMA MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA 2017 NECTA
Dk Msonde amesema kati ya waliofaulu, wasichana ni 341,020 ambao ni sawa na asilimia 70.93 na wavulana ni 321,015 sawa na asilimia 74.80. Amesema idadi ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 72.76. Dk Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa asilimia 70.36, hivyo kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.40.
Katibu Mtendaji huyo amesema ufaulu katika masomo ya Kiswahili, Kiingereza na Hisabati umepanda kwa asilimia kati ya 4.25 na asilimia 10.05 kulinganishwa na mwaka 2016. "Kwa masomo ya Sayansi na maarifa ya jamii ufaulu umeshuka kwa asilimia kati ya 3.56 na asilimia 13.97 kulinganisha na mwaka 2016. Kati ya wanafunzi 909,950 waliofanya mtihani, ni wanafunzi 22,972 pekee sawa na 2.52% ndiyo waliofaulu kwa daraja A.
"Watahiniwa wamefaulu zaidi katika somo la Kiswahili ambalo ufaulu ni asilimia 86.86 na somo walilofaulu kwa kiwango cha chini zaidi ni Kiingereza, lenye ufaulu wa asilimia 40.30," amesema Dk Msonde.
St Peter iliyopo Kagera, St Severine (Kagera), Alliance (Mwanza), Sir John (Tanga), Palikas (Shinyanga), Mwanga (Kagera), Hazina (Dar es Salaam), St Anne Marie (Dar es Salaam), Rweikiza (Kagera) na Martin Luther (Dodoma).
Amezitaja shule 10 ambazo hazikufanya vizuri kuwa ni;
Nyahaa ya Singida, Bosha (Tanga), Ntalasha (Tabora), Kishangazi (Tanga), Mntamba (Singida), Ikolo (Singida), Kamwala (Songwe), Kibutuka (Lindi), Mkulumuzi (Tanga) na Kitwai A (Manyara).
Halmashauri kumi bora kitaifa ni;
Kinondoni (Dar es Salaam), Moshi(M) (Kilimanjaro), Arusha(M) (Arusha), Ilala(M) (Dar es Salaam), Mafinga Mji (Iringa), Mlele (Katavi), Kigamboni (Dar es Salaam), Nzega Mji (Tabora), Mpanda (Katavi) na Chato (Geita)
Aliitaja mikoa iliyoongoza kitaifa kuwa ni;
Dar es Salaam, Geita, Kagera, Iringa, Kilimanjaro, Njombe, Arusha, Mwanza, na Katavi.
Dk Msonde amesema mikoa iliyofanya vibaya ni;
Singida, Tanga, Tabora, Songwe, Lindi na Manyara.
- Ibrahim Shaban - Tusiime (Dar es Salaam)
- Kadidi Mkama Kadidi- Paradise (Geita)
- Acius Job Missingo - St. Peter Claver (Kagera)
- Mahir Ally Mohamedy - Feza (Dar es Salaam)
- Mbarak Faraj - Feza (Dar es Salaam)
- Philemon Damas - St. Achileus (Kagera)
- Huruma Godfrey - Mwanga (Kagera)
- Hamza Azael Almas - Hazina (Dar es Salaam)
- Gibbons Roy - Fountain of Joy (Dar es Salaam)
- Erastus Joseph - St. Peter Claver (Kagera)
- Hadija Aziz Ally - Sir John (Tanga)
- Naseem Kareem Said - Sir John (Tanga)
- Insiyah Kalimuddin Ally - Sir John (Tanga)
- Colletha Masungwa - St. Achileus Kiwanuka (Kagera)
- Linah John Lameck - Sir John (Tanga)
- Saada Ahmed Omary - Sir John (Tanga)
- Khadija Salim Omary - Sir John (Tanga)
- Hannat Ramadhani - Dar-Ul-Muslimeen (Dodoma)
- Efrosina Geofrid - Omukaliro (Kagera)
- Nancy Elirehema Mejooli - Tusiime (Dar es Salaam)
Watahiniwa kumi bora kitaifa ndio hawa hapa;
- Hadija Aziz Ally - Sir John (Tanga)
- Naseem Kareem Said - Sir John (Tanga)
- Ibrahim Shaban - Tusiime (Dar es Salaam)
- Kadidi Mkama Kadidi- Paradise (Geita)
- Acius Job Missingo - St. Peter Claver (Kagera)
- Insiyah Kalimuddin Ally - Sir John (Tanga)
- Colletha Masungwa - St. Achileus Kiwanuka (Kagera)
- Mahir Ally Mohamedy - Feza (Dar es Salaam)
- Mbarak Faraj - Feza (Dar es Salaam)
- Philemon Damas - St. Achileus (Kagera)
Leave a Comment