MSANII WA NIGERIA “DOXY” AFANYA “KIRIKUU REMIX” YA MONI WA CENTRAL ZONE

Wakati wasanii wengi wa Bongo wakijaribu kutafuta wasanii kutoka nje ya Tanzania kujaribu fanya nao kolabo hali imekuwa tofauti kidogo kwa msanii Moni wa Central Zone ambaye ngoma yake ya Kirikuu inaendelea kufanya vizuri kwa radio nyingi nchini Tanzania na hata nje ya mipaka ya Tanzania katika nchi kama Kenya, Uganda, Rwanda, Zambia, na Afrika ya kusini hadi kufikia...

...msanii kutoka Nigeria anayefahamika kwa jina la Doxy kuifanyia ngoma hiyo remix ambayo hivi karibuni itaanza kusikika katika radio station mbalimbali nchini Tanzania na Nigeria.
Msanii Doxy ambaye anatamba na ngoma yake “Roadblock” aliyomshirikisha Clever Tee alipata kuisikia ngoma hiyo kupitia mtandao na akajaribu kumtafuta Moni bila mafanikio ndipo alipokutana na mmoja kati ya watu wa karibu wa Moni kupitia twitter na akaomba kuifanyia remix ngoma ya Kirikuu baada ya kuunganishwa na Moni. Beat ikatumwa nchini Nigeria na bila ajizi Doxy akafanya yake na kuituma ngoma Tanzania baada ya kuifanyia kazi.
Hii ni hatua moja kubwa sana kwa muziki wa Tanzania kwani hii inaonyesha kuna watu kutoka nje ya Tanzania wanafuatilia muziki wetu na wanaupenda hadi kufikia kuomba kufanya kazi na wasanii wa Bongo. Ndiyo maana hata wa’Congo wengi wanakuja fanyia muziki wao Tanzania. Kuwa miongoni mwa wajanja wa kwanza kabisa kuisikiliza ngoma hii pindi inatoka kwa kum’follow Moni kwa instagram, anatumia: Moni_Centrozone na pia waeza kumfollow msanii Doxy kutoka Nigeria kwa twitter anatumia: Doxy

No comments

Powered by Blogger.