HII NDIYO NGOMA AMBAYO ILIMFANYA FID Q ABADILISHE MISTARI BAADA YA KUSIKIA VERSE YA MANGWEA

Ukiisikiliza vizuri ngoma ya marehemu Albert Mangwea inayokwenda kwa jina la Speed 120 alimshirikisha Chidi Benz, kuna mstari kwenye hiyo ngoma Ngwea anasema "na hata nikifa leo pengo langu halina spea". Maneno haya unaweza kuyachulia poa lakini yana ukweli mzito ndani yake kwa mashabiki wa Muziki Muzuri kwani toka Ngwea amefariki dunia hakuna msanii ambaye mpaka leo anaweza fananishwa nae kwa aina ya muziki na staili yake.

Fid Q alishawahi kusema kwa maneno yake kuwa ngoma ya CNN aliyofanya na Ngwea ilimfanya abadili mashairi yake baada ya kusikia mistari na staili aliyopita nayo Ngwea kwenye hiyo ngoma. Hebu fanya kuisikiliza kwa danta uone jinsi Ngwea alikuwa mnyama kiasi gani.
Mangwair ft. Fid Q - CNN from TZhiphop on Vimeo.

No comments

Powered by Blogger.