JINSI YA KUFANYA MEDITATION NA FAIDA ZAKE KWA AFYA
Meditation: Ni ile hali wakati mawazo yanapokuwa yameyeyushwa na kufikia mahali ambapo hakuna fikra yenye kuingia tena.
¡¤ Wengine wanaielezea tahajudi kwamba, ni sala za usiku wa manane.
FAIDA ZA MEDITATION
1. Husaidia kuratibu msukumo wa damu pamoja na usafirishwaji wa damu mwilini.
2. Husaidia pumzi pamoja na kurahisisha usagwaji wa chakula mwilini.
3. Husaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwilini.
4. Husaidia kuleta furaha ya nafsi.
5. Husaidia kuimarisha nguvu yako ya machale pamoja na nguvu zako za ziada.
6. Husaidia kutibu matatizo mengi ya kisaikolojia kwani hubadili hali ya mfumo wa fahamu na mawazo (endapo itafanywa kila siku).
7.meditationpia inaweza kutumika kuomba kitu unachohitaji,kamavile kazi au mahitaji mbalimbali,
Hatua zinazotakiwa wakati unajiandaa kufanya meditation ni kama ifuatavyo:
1. Tafuta sehemu iliyotulia, isiyo na makelele. Kaa kwenye kiti au chini, au lala kitandani. Hakikisha huumii mahali popote. Legeza mwili wako pamoja na misuli yote ya mwili wako kwa kadri utakavyoweza.
2. Sahau matatizo yako yaliyopita, yaliyopo na yajayo. Sahau matatizo yako ya kazini au nyumbani. Jitahidi usifikirie chochote.
3. Ni muhimusanakujali hisia zako wakati unafanya tahajudI.
4. Pumua kwa kuingiza pumzi ya kutosha mapafuni, halafu toa pumzi yote na kufanya kifua kiwekamakitupu. Weka mawazo yako yote kwenye pumzi zako.
Aina za Meditation
1. Meditation ya pumzi.
Ni kongwe zaidi. Ilianzia china na India. Ni tahajudi nzuri au muhimu kwa wale wanaoanza kujifunza.
2. Meditation ya mkono:
Hii inakuonyesha ni kwa jinsi gani mawazo yako yana nguvu zaidi kuliko mwili. Lakini pia inakuonyesha uhusiano uliopo kati ya mawazo yako na mwili wako.
3.Tahajudi ya namba:
Hapa, unatakiwa kuhesabu namba kinyumenyume huku ukiwa umefumba macho. Unaweza ukaanzia 100, 99, 98, 97, 96, ¡-mpaka 1, au unaweza kuanzia 200, 198, 196, 194, 192, ¡-mpaka 2. hakikisha wakati unahesabu namba hizi hukosei, na ikitokea ukakosea namba yoyote hata
kamaumekaribia kumaliza, itakulazimu kuanza upya. Tahajudi hii ni nzuri sana kwa kurejesha kumbukumbu, ingawa pia ina faida nyingine.
Hizo ni baadhi ya tu ya aina za meditation.... By Rakims
Leave a Comment