MAAJABU!! JIJI LA MOMBASA HALINA STAND YA BUS
Mji wa Mombasa ni mmoja wa miji yenye kusifiwa sana kwa mambo mazuri,
nilibahatika kufika pale wiki kadhaa nyuma lakini ajabu niliyoona mji ule hauna hata Stand ya Bus, yaani kila kampuni inapakilia abiria ofisini kwake. Nikamuuliza mwenyeji wangu kulikoni? kaniambia mabepari walishauza kila kitu hata viwanja vya wazi hakuna,nikashangaa kuona hata daladala (Matatu) zao hazina stand zinapakia kokote tu. Ukweli mpangilio wa mji ule uko hovyo kabisa kwa mjini pale labda pembeni ambako sijatembelea.
Kitu kimoja tu nilipenda mji ule pale kivuko cha LIKONI pale wana ferry kama 3 au 4 zinapishana na watu wanapanda bure tu ila magari na vyombo vingine ndio wanalipa.Kwa hilo hongereni sisi hapa tuliambiwa kama hatuna pesa tupige mbizi tu. Kingine barabara ya kutoka horohoro kwenda MSA ni mbovu hovyo kabisa na nyembamba mno. Na nilichoona kingine Kenya maendeleo yao mengi ni ya mkoloni tu lakini toka wapate uhuru sidhani kama kuna la maana wamefanya. Kingine maisha ni magumu sana sana nchi ile jamaa wana dhiki vibaya sana,najiuliza wao kuwa vinara wa Afrika Mashariki kwa uchumi imara lakini uchumi wao hauna faida wala msaada kwa raia wa kawaida.
Chanzo: JamiiForums
Leave a Comment