SIKU AMBAYO BBC ILIKOSA HABARI ZA KUTANGAZA

Imekuwa kama ada kwamba kila wakati lazima kuwe na habari. Lakini zamani, hali ilikuwa tofauti kabisa. Miaka 87 iliyopita, mnamo 18 Aprili 1930, msomaji wa habari katika BBC alikosa cha kutangaza. Taarifa aliyoisoma wakati wa taarifa ya habari ya saa tatu kasorobo usiku ilikuwa: "Hakuna habari". Baadaye, kinanda kilichezwa kwa dakika 15 zilizosalia ambazo zilikuwa zimetengewa habari.

Baadaye, matangazo yalipelekwa Ukumbi wa Malkia katika jumba la Langham Place, London ambapo kulikuwa na tamasha la muziki wa Wagner. Miaka 87 baadaye, hali ni tofauti kabisa. Jumanne ilikuwa siku iliyojaa habari tele. Watu walipokuwa wanashiriki pilkapilka za hapa na pale baada ya Pasaka, Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May aliitisha kikao saa tano mchana na kuahidi kutoa tangazo muhimu.

Wengi walianza kutafakari tangazo lake lingekuwa nini - hadi pale alipotangaza mpango wa kuitisha uchaguzi wa mapema tarehe 8 Juni. Kulikuwa pia na mzozo kati ya Marekani na Korea Kaskazini ambao umekuwa ukitokota kwa wiki kadha sasa. Soma zaidi
Chanzo: BBC Swahili
Leave a Comment