ANGALIA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE 2018)

Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (NECTA) leo Januari 30, 2018, limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne (CSEE) na Maarifa (QT) uliofanyika mwishoni mwa mwaka 2017 ambapo kiwango cha ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 7.22 ikilinganisha na mwaka 2016.

Akitangaza matokeo hayo mbele ya waandishi wa habari, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dk Charles Msonde ameeleza kuwa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 7.22 huku watahiniwa 265 wakifutiwa matokeo kwa udanganyifu wakiwemo wanafunzi 136 waliofanya mtihani wa kujitegemea (Private Candidate) na 129 waliofanya mtihani wa shule (School Candidate).

“Jumla ya Watahiniwa 287,713 ambao sawa na asilimia 77.09% kwa shule za kawaida na vituo vya kujitegemea wamefaulu ambao katika ya hao wasichana wapo 143,728 sawa na asilimia 75.21% wakati wavulana wapo 143,985 sawa na asilimia 79.06%. Mwaka jana wanafunzi waliofaulu mitihani ya kidato cha nne walikuwa 277,283 ambao ni asilimia 70.09% hivyo ufaulu wa jumla umeongezeka kwa asilimia 7.22,” alisema Msonde.

Akitangaza matokeo leo jijini Dar es Salaam, Katibu mkuu wa baraza la mitihani Dr Charles Msonde amesema;

Katika mtihani huo kulikuwa na watahiniwa 385, 767; wasichana wakiwa ni 198,036 sawa na 51.34% huku wavulana ni 187,731 sawa na 48.66%.

Katika mtihani huo watahiniwa wa shule walikuwa 323,332 na wa kujitegemea 62,435
Watahiniwa wa shule 317,777 sawa na 98.28% ndiyo walifanikiwa kufanya hiyo mitahani.
Wahiniwa wa kujitegemea 57,173 sawa 91.57% ndio waliofanikiwa kufanya mitihani. Mtihani wa maarifa 13,775 sawa 84.62% ndio waliofanikiwa kufanya mitihani.

Dr Msnde ameongeza kuwa, watahiniwa 287,713 sawa na 77.09% wamefaulu mitihani yao ya kidato cha nne kwa mwaka 2017 huku wasichana wakiwa ni 143,728 sawa 75.21% na wavulana ni 143,975 sawa 79.06%. Tathimini inaonyesha ufaulu wa watahiniwa wa shule mwaka 2017 umongezeka kwa 7.22% huku ufaulu wa watahiniwa wa kujitegemea mwaka 2017 ukiongezeka kwa 6.22% na ufaulu wa watahiniwa wa mtihani wa maarifa mwaka 2017 umongezeka kwa 9.63%
Watahiniwa 10 waliofanya vizuri na shule wanazotoka ni kama ifuatavyo;

1. Felison Mdee -Marian boys
2. Elizabeth Mango -Marian girls
3. Anna Benjamin Mshana - Marian girls
4. Emanuel Lameck Makoye -Ilboru
5. Lukelo Thadeo Luoga-Ilboru
6. Fuadi Padic -Feza Boys
7. Godfrey Mwakatage -Uwata
8. Baraka Mohammed -Angels
9. Lilian Moses Katabaro -Marian girls
10. Everlyn Moses Mlowe -St. Fransis Mbeya

Dr Msonde amemalizia kwa kubainisha kuwa ufaulu wa jumla kwa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2017 umeongezeka kwa 7.7%.

MATOKEO LINK 1: BOFYA HAPA

MATOKEO LINK 2: BOFYA HAPA

Unaweza kupakua mobile app za matokeo kupitia playstore kwa kubofya

MATOKEO  ya Darasa la NNE - Click Here

MATOKEO ya Darasa la SABA - Click Here

MATOKEO ya Kidato cha PILI - Click Here

MATOKEO ya Kidato cha NNE - Click Here

MATOKEO ya Kidato cha SITA - Click Here

No comments

Powered by Blogger.