JIFUNZE VISA NA MBINU ZA KUKABILIANA NA WEZI WA MAJUMBANI

Napenda tujifunze mbinu mbali mbali za ku deal na wezi na vibaka majumbani na maofisini kwetu. Miongoni mwa mambo yanayorudisha nyuma maendeleo ya binadamu ni ishu nzima ya kuibiwa na wezi kama vibaka, majambazi na hata ndugu au jamaa zetu wa karibu tunao waamini.

Kumbuka nyakati hizi Vijana wengi na watu wazima wamekuwa wakijinyima sana na kujitahid kujenga walau ka sehemu ka kujisitiri (nb:hakuna baba /mama mwenye gari bali kuna baba /mama mwenye nyumba), sasa wengi wakiamia kwenye miji yao baada ya muda mfupi au baadae sana wanakuja kuwa wahanga wa wizi. Hapa uzi huu hata wale waliopanga kwenye hizi nyumba za kupanga unawahusu.

Baadhi ya mbinu ni kama zifatazo:

1- Kusali /kuswali na kuomba kwa Mungu /Alah kabla ya kulala.
Jitahidi kusali na kuomba kwa imani yako na wanafamilia yako, na sio kulala kama wapagani. Mungu ana nguvu sana ya kuweka invisible security kwa mji wako. Usipuuze, kama ni mkristo au muislamu naamini wajua nguvu ya sala / swala kabla na baada ya kulala. Utaleta mrejesho wake hapa .

2- Uimara na ubora wa madirishaNa milango ya nyumba husika.
Hapa Hakikisha madirisha (hasa ya jikoni , stoo , chooni na kwa watoto yako imara sana) ,epuka kujenga kwa kutumia flat bars pekee hasa hzi za MM4 au 4.5 ,6 mimi nakushauri jenga dirisha lako kwa kutumia nondo nzito kabisa afu hizo nondo waweza weka urembo wako unaotaka. Hizo flat bar zinakunjika kama aluminium tu wezi wakija ila nondo watakuwa na kazi ya ziada kuikata, kuipinda hata kuiyeyusha kwa gesi. Waweza shituka mapema ukawadhibiti.pia zege la kutosha na zito kwa madirisha na milango (hapa kwenye ujenzi wengi tuna puuza nguvu ya cement bzito na sio ya kuchakachua wakati wa kubandika madirisha na milango. Pia Milango ya mninga au mpingo ni mostly recomended. Epuka milango ya bei chee na isio imara.

3- Weka master switch itayokuwa pembeni ya kitanda cha kulala.
Hii mbinu ni nzuri sana na wengi mwaweza kuwa hamuijui, unapoweka wiring na switch za nyumba yako, weka na hiyo main switch ya kuweza kuwasha na kuzima taa zote za nje ya nyumba na hata ndani fasta fasta , ukisikia kitu hakiko sawa kwa nyumba yako, usipuuze mara nyingi huwa kweli , hivyo waweza Nyoosha tu mkono wako kitandani bila hata kuamka kitandani na kuzima kwa muda na kuwasha taa zote ...washa zima wezi wanashituka na kujua kuwa huyu yuko macho , ukizima taa zote unawapoteza kabisa. Maana kuna ile uko usingizin unahisi kama kuna watu au kitu kwa nyumba yako hakiko sawa, basi wewe zima taa zote kisha washa na kuzima...nakwambia watabaki wanajiuliza kama hilo tendo ni bahat mbaya au uko macho. pia Usipende kulala taa za vyumbani zinawaka.
Nb: weka main switch vyumba vyote vya watoto, master na chooni kwa master yako. Waelimishe matumizi yake na usiri wake.

4- Weka alarm kwa vitasa na makufuli ya milango na madirishani.Bila kusahau kuwa na filimbi yenyr mlio wa maana.

Inakuwa ni automatic alarm , yaani mlango hata uwe mzuri vipi na vitasa vyake, weweza ongeza na kufuli za alarm (hapa wenye maduka makubwa na magari wanafahamu ) wanaelewa umuhimu wake. Yaani akigusa tu mlango au dirisha na kutumia nguvu kuingia basi alarm au king'ora kinapiga hatari kiasi kwamba mtaa mzima wanashituka. Hayo makufuli yapo na alarm zake zipo hapa mjini, tena usiku mnene sauti yake inasambaa sana. Hata wakikupiga dawa ya usingizi alarm inatibua dili lao haraka sana.
Ila pia firimbi ni muhimu iwe karibu na kitanda ila eneo la siri. Inasaidia sana kutibua mipango ya wezi.

5- Jitahidi kuwa Na baruti au kingo'ra ndani ya nyumba yako.
Waweza kuwa unashangaa, ika nakwambia baruti (gunpowder) inasaidia sana, ukihisi kitu kisicho cha kawaida ukiipiga aisee lazima watafutane kwanza hao wezi (wanaweza hisi kuwa una miliki manati ya mzungu kumbe ni baruti tu). Inakuwa pembeni ya unapolala baba na mkeo. Kumbuka, ukiwa nayo inakuwa siri ya wewe na mkeo tu, tena ikibidi kainunue hata mkoani mbali kabisa. Na king'ora cha kuwatibulia ishu yao, majirani pia watashituka.
6- Weka shoti ya kurusha au kutetemesha kwa milango na madirisha. Na fence ya live kuzunguka nyumba yako.

Dirisha zako na milango unaziwekea mfumo wa kupiga shoti hasa kuanzia saa nne usiku mpaka saa kumi na moja alfajili. Isiwe shoti ya kuua, hapa nazungumzia ule umeme unaoshitua tu, tahadhari, hapa usiwekewe na vishoka watu wa umeme mnanielewa, fata taratibu za nchi na mamlaka zake. Waelemishe pia wanafamilia wako kuacha kugusa madirisha na milango usiku mnene. Najua hii ni ngumu sana , ila nzuri ukiweza masharti yake.

7- Toa elimu ya kujilinda kwa wanafamilia yako wote nyumbani.

Hapa kosa kubwa huwa ni pale baba anapojipa jukumu la ulinzi na usalama wa nyumba yake yeye mwenyewe peke yake (kidole kimoja hakiui chawa), kuwa una wapa elimu mke , watoto na hata beki tatu namna ya kuishi kwa tahadhari hasa nyakat za usiku, ikitokea hatari wafanyeje na pia saini au viashiria vya kuwasiliana na wana familia yako na majirani pia, hii husaidia sana wakat wa majanga ya wizi.

8- Ishi na majirani na wanafamilia yako vizuri.
Ushirikiano na wenzako unao ishi nao kila siku ni muhimu sana , hata kama una pesa zako au una hali ngumu, dont under estimate the power of neighborhood . Dharau na majivuno hayafai, wanaweza ona kitu kibaya kinaendelea kwako hasa wizi wakakaa kimya kutokana na tabia zako.

9- Usilale kama pono samaki usiku.
Jitahidi kulala kisungura usiku, na jiwekee utaratibu wa kutokulala kimoja amka hata mara moja na ku survey nyuma yako , kumbuka ushakua mtu.mzima mambo ya kulala kama mtoto alalavyo uache. Kumbukeni wazee wetu wa zamani walivyokuwa makini na kulala hata kama kafanya kazi ngumu mchana kutwa.

10- Punguzeni ulevi kupindukia.
Watu wengi wanalalamika kuibiwa wakati wao wanashinda baa tena wakinywa mapombe makali makali tu, akirudi nyumbani analala kama furushi la viazi vya njombe..lazima tu wakuchoree raketi maana wanajua unarudi saa sita hivyo mida ya saa nane unakuwa ulimwengu mwingine kabisa, wanazama wanafanya yao.

11-weka ulinzi wa mbwa na hata security guard kama kamera CCTV na bloototh kwa vifaa vyako.

Pale inapokuwa hali yako ya kiuchumi yaruhusu. Fuga mbwa wakali wa kisasa (sio jibwa koko) hasa ndo walengwa pitbull, germanshepherd, na pia weka mlinzi ako trained kwa ulinzi na sio babu wa miaka 70 kwajili ya cheap labor...cheap always cost a lot. Pia kamera za siri chumbani ,sebureni au jikoni ni.muhimu sana kuwepo.

12- Kuwa na silaha ndogo ndogo ndani mwako.

Hasa karibuya kitanda , vitu kama panga (lenye kutu kali na lenye makali ya ncha mbele), jambia (sword), visu vya kubonyeza Kisha kinafumuka kisu kirefu chenye makali upande na upande kama msumeno., Spray za pili pili kali na hata ikibidi tindi kali , bila kusahau mkuki wenye sumu ya nyongo ya mamba (huo umasaini unapatikana sana) , ili kwamba Ukihisi kuna wezi basi uweze jihami kwa silaha hizo.

13- Kuweka gadget za seurity kwa vifaa vyetu muhimu nyumbani.

Hapa vitu kama falt screen t.v ,computer, radio, simu, na vinginevyo vyaweza wekewa tracing gadget kiasi kwamba vikiibwa waweza trace na kufanikiwa kuvidaka kisha ukapata mwizi wako. Hapa yakupasa kuwa una andika baadhi ya fitures muhimu za vity vyako (kwa waliopitia kamali wanajua kitu yaitwa macho kwa karata) kwa diary yako ina case ukimkamata unaanza kutaja alama na baadhi ya taarifa muhimu kwa kitu chako. Sio una nunua kitu cha thamani aafu vikiwekwa hapi 2 vinavyofanana unashindwa tofautisha , utakuwa uzembe na uzururaji.

14- Kuwa mtu wa mazoezi na sio kuwa mzembe mzembe ka dan mtoto wa mama.

Hasa madingi na vijana wa siku hizi wazembe sana kazi kufuga vitambi tu...fanyeni mazoezi uwe fiti kiakili na kimwili.

15- Kuleni chakula cha usiku mida ya usiku wa manane na kwa ratiba maalumu.

Simaanishi kuka ugali maharage saa nane usiku, lahasha ,hapa ina wahusu wana ndoa, acheni tabia Ya kubanjuka kila baada ya kumaliza kula, pumzikeni kwanza kisha muamshe popo kuanzia saa saba au nane usiku. Hakika wezi wakija watawakuta mko macho , hapo ndo watapokuwa wanasonya na kuondoka wenyewe kwa jazba. Na pia sio kukamuana kwa fujo kila siku, mnachosha sana miili kiasi kwamba mkilala ni kama dead body..kulaneni kwa ratiba maana hiyo kitu si mchezo.
Mkimaliza mtalala kama gunia la mbaazi.

16- Usipende karibisha kila mgeni ndani mwako.
Fatilieni wenye nyumba zao za maana wanavyokuwaga na tu viti nje kama ka kijibanda ka makuti basi kanawekwa viti viwili vitatu mnaweza kunywa nakupiga soga lenu na hata kunywa hapo hapo nje bila ya kuingia ndani kwako. Haoa unadhibiti wachora ramani wakipata upenyo wa kukaribishwa ndani (na wengi tunalizwa hapa pasipo kujua), wena usipitilize na kama ikibidi basi kutana na marafiki na jamaa viwanja vya mbali kama baa au beach au hotel hata ikibidi beba familia yako mkamalizana mbali mbali. Pls trust no body.

17- Kuwa makini na madarari wa nyumba, mafundi (ntawataja), wenye nyumba na wale wanaobeba mizigo yetu siku ya kuhama.

Tulio panga tuna dhani tumemaliza kazi kwa kumuamini sana dalali anayejua in and out ya nyumba au chuma chako, pls kuwa makini. Watu hawa maana waweza uza ramani ya nyumba yako.kwa wazee wa kazi. Angalieni sana mitandaoni watu wanaiacha nyumba in and out...sasa wewe ukiingia wajiona.umemaliza Unapigwa tukio unashindwa unganisha dots...
Mafundi ujenzi wa nyumba zetu, mafundi milango na madirisha, mafundi umeme, boda boda na watu wengine wote ...tuwape kazi zetu ila tukae nao kiintelijensia , usimwamini sana kama mkeo au mumeo, wengi wameumiza watu, mpe kazi ikiwezekana under close or regular supervision.
Wenye nyumba nao mmmmh...wengine ukakasi wanakuchora tu.unavyoingiza mavitu ya thamani, mwisho wa siku wana kuchomesha kwa.wana wanafanya yao na wao kugawana mgao.

18- Mwizi ukimdaka mpe kichapo na adhabu heavy mpaka iwe historia kwake maisha yake yote.

Endapo utafanikiwa kumkamata mwizi wako wakati akitenda uhalifu wake..mtandike au hata kumuachia alama atazoeda kuwasimulia wenzake na pia kubaki nazo maisha yake yote , ila usiue pls. Ila adhabu zao zipo nyingi tu ..dont kill him/her pls. Ili akawe balozi mzuri huko aendako.

19- Tuweni makini na mademu au ma boyfriend .
Hii ni kwa wote KE na ME , mnakuwa kwenye mahusiano na mwenzio tena ya muda mrefu huku mki share in and out za maisha yenu ya kila siku, afu mkimwagana kuna uwezekano mmoja wenu akamchoresha kwa wana zilipendwa wake hata kama ni baada ya miez 6 au mwaka.
Chamsingi kama umepanga basi hama na eneo mlilokuaa mkiishi na zilipendwa wako na.kama nyumba inavyumba vingi waweza haa.vyumba akihama mpangaji ili tu kuwapoteza maboyaa au ukishindwa kabisa kata nae mazoea kabisa. Na kama umejenga jitahid kuanza kuishi kwa umakini sana kuanzia hapo . Wengi hulizwa na wandani wake kama tu njia ya kumkomoa.

20- Kuwa una lala usiku kwa kuweka miziki yenye tungo tata kwa sauti ya chini.
Sio kuweka.miziki laini laini kama ya blues...mwanaume wa kweli unaweka miziki migumu Usiku (yakupasa kuwa na kaflash kako au cd maalumu )yenye compilation ya nyimbo zenye tungo tatanishi kwa wezi mfano mimi nina flash yenye nyimbo kama:
(a)sijalal mwangu Utauwawa bureeee....,
(b)itakuwahuzuni kwa ndugu na masela safari yako itavyofika ya kwenda ahela..kamanda wa daz nundaz
(c)kama noma na iwe noma sikubali leo nalivenji mimi...
(d) mikono juu mwendo wa mateka...
(e) mtaji wa masikini ni nguvu yake mwenyewe...

Nk.
Yaani hiyo hata wakinyemelea dirishani kwako wakikuta nyimbo hizo zinapigwa watakuwa na mawazo sana nini lengo la kuwekewa nyimbo ngumu kama hizo badala ya byimo laini za kusindikiza usingizi. Kumbe ni mbinu zako tu za kujihami.


Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.