MAMBO 13 USIYOFAHAMU KUHUSU MELI YA TITANIC

Ilikuwa meli ya ki british ya kusafiria abiria ambayo ilizama kaskazini mwa bahari ya Atlantic 15 april 1912 ikitokea Southampton kwenda New York city, kulikua na abiria takribani 2224 na wafanyakazi.


YAFUATAYO NI MACHACHE KUHUSU MELI HIYO

1. SWIMMING POOL
Titanic ndiyo ilikua meli pekee ya pili duniani kuwa na swimming pool ambalo maji ya baharini yalichemshwa na mashine, hivyo watu walioga maji ya moto. Ila ni first class tu.




2. MOYO WA BAHARI
Unaikumbuka ile cheni ya almasi kwenye movie ya titanic?, ni kisa cha kweli "The heart of the ocean" kama ilivyoitwa cheni hiyo ya bluu ya almasi alipewa kate Florance Phillips na mpenziye ambaye alikua ameoa, bwana Samuel Morley, wapenzi hawa walikuwa wakienda marekani kuanza maisha mapya. Lakini morley kama Jack wa kwenye movie alikufa meli ilipozama.

3. Meli ya titanic ilipogonga bonge la barafu ilikaa maa mawili na nusu bila kuzama.

4. Abiria wengi walishawishika ama kuamini kua meli hii haikuwezekana kuzama "unsinkable" hivyo kupuuzia tarifa kua meli imegonga barafu, wakaendelea kucheza, kula na kunywa.

5. Bei ya nauli ya titanic ilikua ni $4700 kwa sasa ni sawa na dola laki tano ,sawa na tsh 1,127,307,427.

6. Mtu mmoja aitwaye charles joughin aliweza ku survive maji yenye ubaridi wa 31 kwa sababu alilewa mno kabla meli haijazama.
7. Watu laki moja walikwenda kushuhudia uzinduzi wake may 31, 1911.

8. Wakati wa miezi 26 ya ujenzi wake watu 246 waliumia na wawili kufariki.

9. John Jacob ndiye alikua abiria tajiri zaidi kwenye meli hiyo $85 mill, $2 billion ya leo.

10. Watu wengi walikua na ticket za kusafiri na Titanic siku ilipozama,lakini hawakutaka kusafiri,akiwemo MILTON HERSHEY na ALFRED GWYNNE aliyekufa miaka mitatu baade kwenye meli ya RMS lusitania (huyu ni kama aliandikiwa kufia baharini).

11. Meli hii ilipewa tahadhali za barafu kubwa mara sita katika siku hiyo, kabla ya kugonga barafu.

12. Wanamuziki wali perform kwa masaa mawili yote huku wakiona kabisa meli inazama.

13. Bwana THOMAS ANDREWS mbunifu wa meli hii baada ya ujenzi wa meli aliulizwa na mwandishi wa habari "meli hii ni salama kiasi gani ?" Alijibu "ni salama kiasi kwamba hata mungu hawezi izamisha". Mtu huyu alifia humu kwenye meli siku ya ajali.

Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.