FAHAMU MAMBO YA MSINGI KUHUSIANA NA MTOTO MCHANGA
1. Ni muda gani tangia kuzaliwa anaweza kutoka nje?Hakuna muda maalum ambao mtoto anaweza toka nje, anaweza hata kutoka siku ya pili tu baada ya kuzaliwa. Cha muhimu ni kwamba, uwezo wa mtoto kutunza joto ni mdogo (hasa watoto njiti), hivyo ukimtoa nje hakikisha umemvika nguo na kumfunika ili asipoteze joto kabisa.
2. Ni muda gani tangia kuzaliwa anaweza kuanza kula chakula kingine zaidi ya maziwa ya mama?
Mtoto anaweza kula chakula kingine mbali na maziwa ya mama baada ya miezi 6. Maziwa ya mama yana kila kitu mtoto anachohitaji katika miezi sita ya kwanza bila kuongeza chakula chochote. Baada ya miezi sita mtoto aendelee kunyonya mpaka miaka mi2 au zaidi huku akila vyakula mbalimbali vinavyoshauriwa kufuatana na umri wake.
3. Aogeshwe mara ngapi kwa siku?
Kuoga ni njia mojawapo ya kupoteza joto la mtoto. Ile siku ya kwanza kuzaliwa inashauriwa hasiogeshwe. Kisha waweza kuendelea kumuosha mtoto (epuka maji mengi) kadri inavyohitajika. Ni vyema kumfuta kwa kitambaa kilicholoweshwa maji ya vugu vugu unapombadili mtoto akijisaidia kuliko kumuogesha kila mara.
4. Nini kitamtokea mtoto kama nitaanza kufanya mapenzi na mamake baada ya siku arobaini tangia kuzaliwa na kama sita tumia condom?
Kwa kawaida mwanamke baada ya kujifungua inachukua muda kidogo kurudi kwenye mzunguko wake wa mwezi, hii hucheleweshwa zaidi na kunyonyesha..ndio maana kunyonyesha inachukuliwa kama njia mojawapo ya kupunguza uwezekano wa mimba ya mapema. Ukifanya mapenzi na mama mtoto baada ya siku arobaini ataweza kupata mimba. Akipata mimba mfumo wake wa 'hormoni' hutabadilika na maziwa yatapungua hadi kuisha kabisa, kitu ambacho kinaweza kuathiri afya ya mtoto (ndio wanaita kubemenda, sio kweli manii/mbegu ndio zitamuathiri mtoto kupitia maziwa). Sio mbaya kuanza kufanya mapenzi baada ya arobaini, lakini mtumie 'kondomu' ili kuepusha mimba ya haraka ambayo zaidi ya kuweza kuleta athari kwa mtoto, inamuathiri na mama pia.
5. Na mambo mengine ambayo sijayaorodhesha ila yanaweza kunifaa juu ya mtoto mchanga.
Mambo mengine: mpende sana mwanao na mama yake, spend nao time ya kutosha, hii inamsaidia mama kutulia kiakili na kihisia na kutoa maziwa ya kutosha kwa mtoto, shiriki kumhudumia mtoto (kuchange dippers, nepi, etec), cheza na mtoto ujenge bond, and enjoy fatherhood.
Chanzo: Jayson Jr Facebook.
Leave a Comment