HATIMAYE MSANII 'AY' ATIMIZA NDOTO ZAKE ZA MUDA MREFU
MWANAMUZIKI mkongwe kwenye gemu la Bongo Fleva, Ambwene
Yessaya ‘AY’, ambaye wimbo wake wa Microphone aliomshirikisha Fareed Kubanda
‘FID Q’ ndiyo mpya kwa sasa, amefunguka siri ya kuamua kuishi Marekani..
Akichonga na Star Showbiz, dairekti kutoka kwenye ardhi hiyo ya Donald Trump,
AY mwenye makazi katika Jiji la Calabasas, California alisema ilikuwa ni ndoto
yake ya muda mrefu kwamba siku moja awe na makazi kwenye taifa hilo mbali na
alipozaliwa Tanzania. “Siri ya kuja kuishi Marekani ni kwamba hii ilikuwa ndoto
yangu ya muda mrefu niwe na makazi huku. Kwa hiyo kwa kufanikisha kununua
mjengo Marekani kwangu nimetimiza jambo moja muhimu sana maishani mwangu na
ninamshukuru Mungu,” alimaliza AY.
Leave a Comment