JINSI YA KUMJUA MGANGA AMBAYE NI MCHAWI


Uchawi ni jambo baya na hutakiwi mtu kujifunza wala kumfunza mtu. 

Kwa uchache hapa nawaletea alama za kumjua mganga ambaye ni mchawi,na endapo ukiziona alama hizi basi hutakiwi kutibiwa nae bali wewe unapaswa kuondoka haraka sana na kuachana nae.

1. Kutumia najisi katika matibabu kama mkojo,damu ya hedhi na mfano wake.

2. Kumpa mgonjwa dawa kwa masharti yenye kufungamana na majini,mathalani kumwambia dawa hii nenda kaichimbie makaburini au nenda kapusue hii nazi njia panda.

3. Kujua habari za mgonjwa kabla ya kuambiwa hapo kuna kuwa na mawasiliano na Shetani.

4. Mganga kutaka jina la mgonjwa au wazazi wake hasa mama yake.

5. Mganga kutaka vitu vya mgonjwa mfano kucha zake,nguo zake,nywele zake na mfano wake.
6. Mganga mwenye kutenganisha watu aidha mke na mume,mfanya kazi na muajiri wake au ndugu kwa ndugu huyo nae ni mchawi.

7. Kuandika maneno yasiyo fahamika au kusema maneno yasiyofahamika huyo ni mchawi.

8. Kupewa vitu na ajiitae mganga na kwenda kuvichimbia ardhini,kupeperisha hewani,kuvichoma moto huku ukisema maneno fulani huyo si mganga ni mchawi.

Kuna alama nyingi juu ya jambo hili, kwa leo tuishie hapa, kama ukiwahi kukutana na hizi alama jua ulifanya shirki na unatakiwa kufanya toba ya kweli.

Najua wengi wamekutana na hizi kwa kujua au kutokujua.

Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.