FAIDA ZA KIBALI CHA UJENZI, JINSI YA KUKIPATA NA KITAKACHOKUPATA ENDAPO UTAJENGA BILA KUWA NACHO
Kibali cha ujenzi(Building permit), ni moja ya kanuni muhimu sana ya upangaji wa miji nchini Tanzania. kila anaehitaji kujenga anapaswa kufuata kanuni za kibali cha ujenzi atakachopewa, mara nyingi kwa mujibu wa sheria kibali cha ujenzi hutolewa na mamlaka za serikali ambazo ni halmashauri kupitia idara ya mipango miji na mazingira.
Kulingana na sheria ya ujenzi wa majengo mijini Na 101 ya mwaka 2009 si ruhusa kwa mtu yeyote kujenga au kuanza kujenga jengo bila ya kuwa na;
- Uhalali wa umiliki wa ardhi mahali unapojenga.
- Kibali cha ujenzi kutoka mamlaka husika.
1. UMUHIMU WA KIBALI CHA UJENZI
- Kutimiza matakwa ya kanuni za ujenzi mijini.
- Kuwezesha kujenga majengo ya nyumba kama yaliyoelekezwa katika mipango miji ya sehemu husika.
- Kudhibiti ujenzi holela.
2. JINSI YA KUPATA KIBALI CHA UJENZI
- Kuwasilisha michoro ya ramani ya jengo kwa ajili ya uchunguzi.
- Kulipia malipo stahiki ya uchunguzi wa ramani hizo.
- Kulipia malipo ya kiwanja kwa mwaka husika.
3. JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI MICHORO YA MAJENGO MAALUMU.
Michoro ya majengo maalumu(Maghorofa, kumbi, Taasisi mbalimbali, Bar, Vituo vya mafuta, Viwanda, Hospital na majengo mengine ya jinsi hiyo iwasilishwe kwa kuanza na michoro ya awali ya kisanifu(Preminary Drawings) ambayo itahusisha.
- Michoro ya sakafu(Floor plan) 1:100
- Sura ya jengo(Elevations) 1:100
- Mkato wa jengo(Section) 1:100
Baada ya uchunguzi wa michoro ya awali kukamilika itawasilishwa michoro ya michoro(Final Drawings) ambayo ni michoro ya kisanifu na ya kihandisi(Architectural and structural drawings) kwa ajili ya uchunguzi.
● Michoro inayowasilishwa izingatie kanuni na taratibu zote muhimu za kiuchoraji(Architectural and Engineering Aspects) na iwe imesainiwa na msanifu majengo/Mhandisi anayetambuliwa(Architectural and Structural Endorsement).
● Michoro hiyo iambatane na nakala ya cheti cha uchunguzi wa athari za kimazingira(Environment Impact Assessment EIA).
● Michoro iambatane na nakala za nyaraka zote halali za umiliki wa kiwanja husika pamoja na stakabadhi ya malipo ya kiwanja kwa mwaka husika.
● Michoro yote iwasilishwe ikiwa na maandishi yanayosomeka(Readable text).
● Michoro yote iwasilishwe kwenye ukubwa wa karatasi(paper size) A0,A1,A2 au A3.
4. JINSI YA KUWASILISHA MAOMBI YA MICHORO YA MAJENGO YA KAWAIDA.
Michoro ya majengo ya kawaida itawasilishwa kwa kuzingatia maelezo ya hapo juu isipokuwa haitatangiliwa na michoro ya awali(Preminary Drawing) kama ilivyo katika michoro ya majengo maalumu.
- MICHORO ILIYOANDALIWA IONYESHE NINI.
● Litakavyokuwa(Plans,Sections,Elevations,Foundation,Roof plan,Site plan).
● Ramani ya kiwanja(Location plan).
● Namba na eneo la kiwanja kilipo.
● Jina la mmilikaji ardhi inayohusika.
● Jina la mchoraji, ujuzi na anuani.
● Ukubwa wa jengo kwa mita za mraba.
● Ujazo wa kiwanja(Plan ratio).
● Urefu wa jengo(Height).
● Matumizi yanayokusudiwa.
● Idadi ya maegesho yatakayokuwepo.
● Umbali kwa jengo kutoka kwenye mipaka ya kiwanja(Setbacks).
● Mfumo wa kutoa majitaka hadi kwenye mashimo.
- VIAMBATANISHO UNAVYOTAKIWA KUWA NAVYO.
● Fomu moja ya maombi iliyojazwa kwa usahihi.
● Hati ya kumiliki kiwanja au barua ya toleo.
●Kumbukumbu zingine zinazohusu kiwanja hicho kama hati za mauzo makabidhiano na mengine.
● Nakala ya risiti ya kodi ya kiwanja na kodi za majengo.
● Mabadiliko ya matumizi ya ardhi.
● Ramani ya kiwanja iliyosajiliwa.
- UMUHIMU WA KIBALI CHA UJENZI.
● Kutimiza matakwa ya kanuni za ujenzi mijini.
● Kuwezesha kujenga majengo na nyumba kama yaliyoelekezwa katika mipango miji ya sehemu husika.
● Kudhibiti ujenzi holela.
- MUDA WA UPATIKANAJI WA KIBALI CHA UJENZI.
● Endapo mwombaji atakamilisha hatua zote muhimu kwa wakati atapata kibali cha ujenzi ndani ya majuma mawili(2) hadi manne(4).
● Hii ni pamoja na uwasilishaji wa ramani zilizoidhinishwa na wataalamu husika na hati za umiliki zilizo sahihi.
- WAJIBU WA MWANANCHI.
Ni wajibu wa kila mwananchi kujenga au kukarabati nyumba yake iliyo ndani ya mji/jiji kwa kibali kutoka halmashauri.
- TAHADHARI
● Endapo mwananchi yeyote atajenga au kukarabati nyumba bila kibali cha ujenzi toka halmashauri,atapewa ilani ya kusimamisha ujenzi au ukarabati na kushauriwa kufuata taratibu za kuomba kibali cha ujenzi ndani ya siku saba(7).
● Kama mwombaji atakaidi ilani ya kusimamisha jiji au miji litampa ilani ya kubomoa jengo lake mwenyew na akishindwa jiji litabomoa jengo husika na kudai mmiliki gharama za utekelezaji wa ubomoaji.
Imeandaliwa na; UTUKUFU CLEMENT MWANJISI
(Planning officer wa kujitegemea).
Leave a Comment