UKWELI KUHUSU "MALAIKA" ALIYEANGUKA UINGEREZA

Kumekuwepo na picha ikimuonyesha 'Malaika' anayedaiwa kuanguka huko Uingereza hivi karibuni na kuzua gumzo kubwa miongoni mwa watumiaji wa mtandao ambao wanaishia kuona picha bila kufahamu ni nini kilichotokea hadi kufikia 'kuanguka' kwa malaika huyo..! Maswali mengi yamekuwepo na miongoni mwa maswali hayo ni pamoja na.. 
1. Kwanini hajaanguka malaika mweusi?
2. Nguo alizovaa ameshonea duniani ama mbinguni?
3. Akitaka kuondoka je? Itakuwaje?
4. Mbinguni wanajua kama 'malaika' wao ameanguka duniani?
Maswali haya na mengineo mengi yamekuwepo kwa vichwa vya watu wengi tangu picha hiyo ya 'Fallen Angel" kusambaa. Ukweli wa mambo ni kwamba, yule aliyenguka sio 'malaika' kama ambavyo imekuwa ikisemekana bali ni kazi ya wasanii wawili wa kichina Sun Yuan na Peng Yu ambao walitengeneza mfano wa malaika aliyeanguka na kwenda kuonyesha katika maonyesho ya Saatchi Gallery yaliyofanyika London, Uingereza.
Wasanii hawa wa kichina wanafahamika kwa kazi zao nyingi ambazo zinaonekeana katika hali ya uhalisia ingawa ni kazi za kubuni. Kazi nyingine ziliyofanywa na wasanii hawa ni hiyo hapo chini, ambapo nazo zilikuwepo kwenye maonyesho.

No comments

Powered by Blogger.