BAADA YA DIAMOND PLATNUMZ NA WEMA SEPETU, SASA NI ZAMU YA MILLARD AYO

Mtandao umesaidia kwa kiasi wasanii kufikisha kazi zao mbali zaidi na pia kujitangaza kwa biashara za wafanyabiashara mbalimbali nchini Tanzania na duniani kote. Kupitia mtandao wa instagram, msanii Diamond Platnumz na aliyekuwa miss Tanzania ambaye kwa sasa ni C.E.O wa Endless Fame, Wema Sepetu ndiyo watu pekee nchini Tanzania ambao wana followers zaidi ya millioni moja (1M). Kwa Afrika wasanii (muziki / maigizo) ambao wamefikisha followers zaidi ya millioni moja ni pamoja na Davido (@davidoofficial), WizKid (@wizkidayo), Diamond Platnumz (@Diamondplatnumz) na Wema Sepetu (@wemasepetu). Millard Ayo ambaye ni mtangazaji wa Clouds Fm ambaye kwa sasa ana studio zake binafsi ambazo anatumia kurekodia vipindi vyake ambavyo vinasikika katika nchi mbalimbali Afrika mashariki na kati atakuwamiongoni mwa watu...


...ambao wamefikisha followers millioni moja (1M) kwa mtandao wa Instagram. Mpaka sasa ana followers 992K ambao ni sawa na followers laki tisa tisini na mbili elfu (992,000) akibakiza watu elfu nane tuu 8000 kufikisha followers millioni. Unaweza kum follow kwa link HAPA kuwa miongoni mwa watu millioni moja ambao wamemfollower mtu wako wa nguvu Millard Ayo ambaye ndiyo mtangazaji ambaye kipindi chake cha Amplifaya kinachorushwa na Clouds Fm kina wadhamini wengi zaidi kuliko vipindi vyote nchini Tanzania.

No comments

Powered by Blogger.