MAKALA ZA UREMBO: NJIA ZA KUFANYA UWE MREMBO SIKU ZOTE
Dhana ya urembo imekuwa na tafsiri tofauti kwa watu wengi. Kila
mmoja anautafakari urembo kwa namna yake kulingana na malezi na mahali alipo.Wako wanaoamini kuwa mrembo ni lazima uwe na ngozi nyeupe,
wengine hudhani kuwa ili kuonekana mrembo, lazima uwe na nywele ndefu, lakini
pia wapo wanaodhani kwamba ili uwe mrembo ni lazima uwe na umbo namba nane.
Hiyo yote ni mitazamo tu, lakini tafsiri halisi kutoka kwa wataalamu wa urembo ni kwamba; urembo ni hali ya kuwa na afya bora.
Hiyo yote ni mitazamo tu, lakini tafsiri halisi kutoka kwa wataalamu wa urembo ni kwamba; urembo ni hali ya kuwa na afya bora.
Kabla hujafanya chochote kuhusu afya yako, unatakiwa kuamini
kwamba wewe ni mrembo. Ikiwa utasimama katika hilo ni kweli utakuwa mrembo siku
zote.
Safisha ngozi yako
Hakikisha ngozi yako inakuwa safi muda wote. Unaweza kutumia njia mbalimbali
kama vile kuondoa ngozi zilizokufa mara kwa mara. Kuondoa mafuta
yaliyogandamana katika ngozi kwa kufanyia masaji ngozi yako ili kurahisisha
mzunguko wa damu yako.
Ikiwa hili litafanyika kwa umakini ni wazi kuwa matatizo ya kuwa na chunusi au
weusi katika ngozi yako havitakuwepo kwako.
Tumia bidhaa za nywele, ambazo zinaendana na nywele zako na
hakikisha unazingatia mambo muhimu katika uboreshaji wa nywele zako.
Miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na
kutokutumia vifaa vinavyounguza vywele.
Epuka kuosha nywele kwa maji ya moto, pia kuchana nywele zikiwa na maji, kwani
unaweza kusababisha kukatika kwa nywele zako.
Safisha meno yako
Usafi wa meno pia ni miongoni mwa mambo ya kuzingatia unapoamua kuboresha
urembo wako. Hakikisha unapiga mswaki walau mara mbili kwa siku kila siku au
kila baada ya kula.
Usipake vipodozi mara kwa mara
Tumia vipodozi pale inapobidi, usipendelee kutumia vipodozi mara kwa mara kwani
wakati mwingine matumizi ya mara kwa mara ya vipodozi, husababisha madhara
katika ngozi yako, hasa unapotumia bila kufuata maelekezo ya wataalamu.
Fanya mazoezi
Hakikisha mazoezi yanakuwa sehemu ya maisha yako, hii itasaidia kukufanya
uonekane siyo tu mrembo, bali pia mwenye kujiamini.
Pata usingizi wa kutosha
Hakikisha unapata usingizi wa kutosha kila siku. Kwa mujibu wa wataalamu,
unatakiwa kulala si chini ya saa nane kila siku. Ikiwa utapata usingizi wa
kutosha ni wazi kuwa macho yako yataonekana yenye nuru siku zote. Pia utazidi
kuonekana kuwa mrembo zaidi.
Imeandaliwa na Maimuna Kubegeya
Leave a Comment