USHAURI WA BURE KWA JOKATE MWEGELO

Mwaka 2014 kuingia 2015 umekuwa ni mwaka wa mafanikio kwa wasanii wengi wa Tanzania hasa baada ya wengi wao kufanya vizuri katika upande wa video na vichupa vyao kupenya katika channeli kubwa Afrika na hata ulimwenguni ukiachilia mbali kupata watazamaji wengi katika mitandao kama Youtube na mingineyo.
Baadhi ya wasanii ambao vichupa vyao vimepata kupigwa na channel kama MTV Base, Trace, Channel O na Soundcity ni kama Asante na Its going down za Ambwene Yessaya "AY", Nobody but me ya Vannesa Mdee, Nusu nusu ya Joh Makini, Siachani nawe ya Baraka Da Prince, Number One (original na remix) na Mdogomdogo ya Diamond Platnumz na nyinginezo nyingi. Haya ni mafanikio makubwa sana kwa muziki wa Tanzania ambapo muziki wa kizazi kipya hauna muda mrefu tangu ukubalike na kupata mashabiki wengi kuliko aina yoyote ya muziki kwa ndani ya Tanzania....

Wakati Vanessa Mdee akitutoa kimasomaso kwa wanamuziki wa kike Tanzania kwa kufanya vizuri nje na ndani ya Tanzania, Jokate Mwegelo hayupo mbali sana katika muziki ingawa ni miongoni mwa wanamitindo na wajasiriamali wenye mafanikio makubwa. Hana historia nzuri sana ya muziki ambayo inaweza kukuonyesha hustlin zake za muziki kama ambazo wamepitia wasanii wengine bali yeye ameweza kutumia fursa aliyopata baada ya kushiriki mashindano ya Miss Tanzania, ingawa hakushinda lakini kwa sasa yeye ni zaidi ya mshindi kwa kutumia vizuri fursa anazopata iwe kimuziki ama kibiashara..
Sasa huu ni ushauri wangu wa bure kwa Jokate Mwegelo ambaye amefanya ngoma inayokwenda kwa jina la "Leoleo" akimshirikisha Ice Prince kutoka Nigeria. Jokate dada'angu, kama ulikuwa huna wazo la kufanya video ya wimbo "Leoleo" naomba ufikirie mara mbili. Ukishapata wazo la kufanya video Ts Ok, kitu cha pili angalia ni nani wataka awe director wako? Kwa mimi kutokana na nyimbo yako, kuna watu watatu Afrika ambao wanaweza kuifanya hii video ikawa international na kuitendea haki nyimbo yako ambayo inawezekana ndio video inayosubiriwa zaidi na fans wa kike baada ya Vannesa Mdee kutoa Nobody but me ambayo video yake na audio song ya Jokate zilipishana siku chache katika kuachiwa. Wa kwanza ni Sesan,huyu jamaa nilianza kumuelewa baada ya kufanya kichupa cha Sarkodie ft Bank W – Pon Di Ting.. yaan utadhani Bedrock ya YMCMB waliiga idea ya mchizi ambaye video ingine amefanya ni Fans Me ya Davido ft Meek Mill. Director wa pili ambaye anaweza kufanya video ya Jokate ikawa bora Clarence Peter, huyu jamaa ni mnoma aisee ile kitu ya P square "personally" ndiyo video ya msanii wa Afrika ambayo imeangaliwa zaidi xoxo Director namba mbili ni Justin Campos ambaye amefanya video ya Vannesa Mdee na Joh Makini. Nimepata kuangalia pia kazi nyingine za Justin Campos ukiacha Nusunusu na Nobody but me, for sure watanzania tunahitaji kuwekeza sana kwenye video kama tunataka kwenda international kuanzia wasanii mpaka production teams.
Endapo utafanikiwa kuifanya hii video, then zillax o chillax wao wasema relax and subiria mchongo wa Ice Prince kusainiwa Roc Nation ukae sawa, kama imetokea umekaa sawa na mchizi "Ice Prince" kapata mchongo wa kusimamiwa kazi zake na lebo ya Jay Z hapo ndo pa kufanya launch ya video ya "Leoleo". Yaani siku Jay Z anatangaza rasmi kumsaini Ice Prince ndiyo siku ya ku launch kichupa kwa misingi ipi ujue? Jay Z ni mmoja wa watu ambao ni 'Talk of the internet' endapo atafanya ishu yeyote ile na kama ambavyo unajua kwamba Lagos Nigeria ndiyo jiji lenye watu wengi zaidi Afrika xoxo hapo Jokate anapata fanbase yenye back up kubwa kichiz kwa sababu fans wengi watataka kumfahamu zaidi Ice Prince na kutaka kujua kazi zake  na ndipo wanapokutana na Leoleo ya Jokate ft Ice Prince. Jokate dada'angu, we kaza siku hizi Rihanna anazingua eti anaita wenzie b*tch afu anawadai hela zake..

Hebu fanya kubofya HAPA kui DOWNLOAD ngoma ya Jokate ft Ice Prince - Leoleo

No comments

Powered by Blogger.