CHANZO CHA BIFU LA MR BLUE NA MR II "SUGU" HIKI HAPA

Mr Blue ni miongoni mwa wasanii kutoka Tanzania ambao wamekuwepo kwenye hili game la muziki kwa kitambo sasa. Hivi majuzi alitoa nyimbo ambayo amemshirikisha Mr II a.k.a Sugu na Miss Lizzy, wimbo unakwenda kwa jina la Freedom. Beat ya wimbo huo imefanywa na Daxo Chali kutoka Mj Records. 
Hivi majuzi Mr II "Sugu" ameurudia wimbo huo na kuufanyia video kabisa kitendo ambacho Mr Blue anakilalamikia kuwa Sugu kamuibia beat yake. Kwa maelezo ya Daxo Chali ambaye ndiye aliyegonga beat hiyo anasema kuwa Blue hana haja ya kulalamika kwani beat hiyo alipewa bure na hata chorus ya wimbo huo alikuta imeshafanywa na Miss Lizzy. Hebu fanya kuicheki video ya Mr II "Sugu" na uisikilize ngoma ya Mr Blue halafu tuambie ipi kali.

Ikumbukwe kuwa Mr Blue alishawahi kumlalamikia Diamond Platnumz kuwa kamuibia jina lake "Simba" ambalo anadai alikuwa analitumia kitambo

No comments

Powered by Blogger.