TUAMBIE KITUKO ULICHOWAHI KUKUTANA NACHO KWENYE FILAMU ZA BONGO, MIE NILIKUTANA NA HIKI...

Kituko ambacho nimekutana nacho juzi kati naangalia filamu ya Bongo ktk channel ya Sinema zetu kimenifanya nisiangalie Filamu hizo tenaaa! Jamaa anakumbukia miaka kumi iliyopita yuko bar anacheza wimbo wa Darassa maisha na muziki, jamani kweli????

Nilizima na main switch kabisa nikaenda kulala... sipendagi ujina mimi

Wengineo walikutana na vituko vifuatavyo:
1. Bibie anafungua geti kwa fujo, anaenda dukani kwa mangi kununua sumu kwa ajili ya kujiua. Cha ajabu anasubilia chenchi!
2. Eti jini anavuka barabara anangalia kulia kushoto tena kulia halafu anavuka.
3. Mke anamwekea mumewe sumu kwenye juice alafu anaonja kama sumu imekolea ila yeye hafi mumewe ndo anakufa.
4. Jambazi anavamia lakini anavua viatu kabla ya kuingia ndani.

5. Jini anakunywa bia daaaah hadi raha aiseee.
6. Kwenye Bongo movie lazima mlinzi wa nyumbani awe mjinga-mjinga.
7. Jambazi ameshika bunduki halafu anasema "ntakuchinja"
8. Jamaa wa miaka 30 kahukumiwa jela miaka 30 kwa kosa la ubakaji cha kushangaza baada ya miaka 30 anatoka akiwa bado kjana vlevle na bado amevaa T-shirt, jeans na raba zile zile alizoingia nazo gerezani. 
Ongeza na vituko ulivyowahi kukutana navyo kwenye Bongo movies..!!


No comments

Powered by Blogger.