MSANII JACO BEATZ ATANGAZA RASMI KUACHANA NA MUZIKI

Msanii kutoka mkoani Dodoma anayefahamika kwa jina la Jaco Beatz kupitia mtandao wa Facebook alitangaza rasmi kuacha kujishughulisha na kazi za muziki akidai ya kuwa atabakia kuwa mdau tuu. 

Jaco Beatz alitamba na nyimbo kama Nimependa Tena alioimba na Wise One, Amazing na Miss You. Haya ndiyo aliyoandika Jaco Beatz kuhusiana na kuacha kwake muziki...!! 
NAtangaza kuachana na shughuli za mziki rasmi leo hii na kubaki kama mdau. ...I hope waliotamani litokee hili wako na amani mioyoni mwao ....nashukuru sana na nawapenda sana dodoma hata siku nikifa nikumbukwe kwa machache niliyotenda.

No comments

Powered by Blogger.