ZIJUE MBINU ZA KISASA ZA KUKWEPA KUMLIPA NAULI KONDAKTA KATIKA DALADALA

  1. Epuka kupanda Daladala ambalo halijaa kwani utaumbuka kiurahisi sana bali subiria Daladala lenye nyomi / lililojaa ndiyo ulipande.
  2. Ukishaona Kondakta anaanza kuchukua nauli jifanye unaongea sana na Simu tena kwa Sauti kubwa huku ukiwa ' Seriuos ' kabisa halafu humtizami Kondakta. Mara nyingi sana Makondakta huwasau Watu ( Abiria ) wanaoongea sana na Simu katika Madaladala hadi kupelekea kusahau kuwadai nauli.
  3. Ikitokea alikupita wakati anachukua nauli akirudi Kwako na kukudai ' mkazie ' mimacho yako huku ukimuangalia ambapo Makondakta wengi hujawa na ' aibu ' kama si ' uwoga ' na kuondoka zao.
  4. Ukiona kaanza kuchukua nauli siti za mbele Wewe anza taratibu kujifanya kama vile unaonyesha unataka kushuka Kituo cha mbele na ukiona unakaribia kukutana nae katikati anzisha ' zogo ' la kuwataka abiria wenzako mliosimama wasogee kisha haraka sana ' Kiaina ' unahamia kule ambako Kondakta ameshamaliza kuchukua nauli.
  5. Pima saikolojia na Dereva na Kondakta wake ambapo ukiona wote wanapenda nyimbo za Seduce Me au Zilipendwa tiririka nazo kwa kuzisifia na kuzizungumzia sana au ukiona Dereva na Kondakta wake wanapenda sana mpira serereka na hizo hizo stori za akina Tshishimbi au Niyonzima na automatically tu utaona Kondakta au Dereva wamejenga Urafiki wa ghafla nawe na watasahau hata kukudai nauli yao.
  6. Pendelea sana kujifanya unasinzia ndani ya Daladala kwani mara nyingi sana Makondakta huwa wakiona Watu wamelala huwapita Kwanza ambapo akishamalizana na kule alikochukua nauli yake akirudi tena huku anakuwa amesahau.
  7. Kama hiyo njia mnayopita ina ' Yange Yange / Matrafiki ' wengi hakikisha kila mnapowapita basi Wewe unajifanya hata tu unawapungia mkono hao ' Matrafiki ' na kila unapomaliza kuwapungia mkono / kuwasalimia hakikisha macho yako yanamtizama Kondakta kitendo ambacho kitamfanya Yule Kondakta ahisi labda Wewe ni Askari au unaweza ' Kumlengesha ' kwa Matrafiki wengine wa mbele hivyo automatically tu utaona anakupita au hata akikupigisha stori lakini akiwa ni muoga muoga na hatothubutu kukuomba nauli.

ANGALIZO.
Hizi mbinu zitanoga endapo tu na Wewe basi mfukoni mwako una hata akiba ya Tsh 800/=. lakini kama ukizitumia halafu dili ' likabuma ' na ukashtukiwa unaweza ukaumbuka vibaya na kuishia tu Polisi na kufanya Kazi ya kufagia na kupiga deki hadi jioni.

Nawatakieni ukwepaji ulipaji nauli mwema Kesho asubuhi kwa tunaoamka na kutumia ' Daladala ' kwa ajili ya usafiri wa kutupeleka katika mihangaiko yetu na kwa wale ambao hizi mbinu Kuu Saba ( 7 ) zitwasaidieni msione aibu kuja kuniletea ' mrejesho / feedback'.


Chanzo: JamiiForums

No comments

Powered by Blogger.