WEMA SEPETU ATANGAZA RASMI KUONDOKA CHADEMA, ARUDI CCM

Msanii Wema Sepetu ambaye hivi majuzi alijiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amejivua uanachama wa chama hicho na kuamua kurudi CCM. Kupitia ukurasa wake wa instagram, msanii Wema Sepetu aliandika "Siwezi Kuendelea kuishi kwenye Nyumba inayo nikosesha amani... Peace of mind is everything for me... Natangaza Rasmi kuondoka Chadema na Kurudi Nyumbani.... #ThereIsNoPlaceLikeHome... Feels good to be Back...."

Hata hivyo, baada ya Wema kutangaza kurudi CCM, msemaji mkuu wa Chama cha Mapinduzi H. Polepole alisema kuwa CCM sio sehemu ya watu kutoka na kurudi vile watakavyo, na akauasa umma kuwa mtu yeyote anayetaka kurudi CCM afate sheria na kanuni za chama na sio vinginevyo...!!
Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.