BAADA YA WIZKID NA DAVIDO KUPATANA, DIAMOND NA ALIKIBA WAUANZA MWAKA KIVINGINE

Mwaka jana mwishoni mashabiki wa muziki duniani kote walishuhudia wasanii wawili ambao ilikuwa inasemekana wa bifu huku media zikikuza bifu hilo na watu wakahisi kweli kulikuwa na ugomvi baina ya msanii Davido na Wizkid wote kutoka nchini Nigeria hadi mwaka jana mwishoni ambapon wawili hao walionekana kwenye stage moja wakiimba kwa pamoja, kama ambavyo unaweza kuona hapo chini kwa video.
Huku Tanzania mambo bado ni 'motooo' kwani hakuna dalili yeyote ya kuonesha manguli wetu wawili Diamond na AliKiba wakipatana au hata kufanya nyimbo moja. Wanaweza kuiga mfano mzuri kabisa kutoka kwa viongozi wetu wawili, mheshimiwa Rais Dr JPM alivyoamua kukutana na Mheshimiwa Lowassa ikulu ilhali wawili hao walishakuwa wapinzani katika kipindi cha kampeni za urais. Lakini wakaondoa tofauti zao na kukutana kisha kujadililiana mustakabadhi wa taifa kama watanzania.
Kwa kuona hivyo basi tunapenda kutambulisha kwenu mobile app yenye kuonyesha nyimbo zote za wasanii hawa (Diamond na AliKiba) ikiwa ni mojawapo ya juhudi za kuwahimiza wawe kitu kimoja ili tuweze kufikisha muziki wetu mbali zaidi. Unaweza kupakua mobile app ya Diamond Vs AliKiba kwa kubofya HAPA

No comments

Powered by Blogger.