MBUNGE WA IRINGA MJINI, MCHUNGAJI MSIGWA AKAMATWA NA JESHI LA POLISI NA KUPELEKWA MAHABUSU


JESHI la polisi mkoani Iringa linamshikilia mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa kwa mahojiano kutokana na matukio ya kiuharifu yanayotokea mjini Iringa. Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa (RPC) Julius Mjengi ameuthibitishia mtandao huu usiku huu baada ya kupigiwa simu kuhusiana na kuzagaa kwa taarifa za kukamatwa kwa mbunge Msigwa katika mitandao ya kijamii.
Kamanda huyo amesema kuwa ni kweli hadi majira ya saa8.25 usiku huu alikuwa akihojiwa juu ya matukio ya uvunjwaji wa nyumba ya aliyekuwa diwani wa kata ya Mwangata kupitia chadema aliyejiuzulu na kujiunga na CCM pamoja na tukio la kuchomwa moto kwa nyumba aliyokuwa akiishi katibu wa UVCCM Iringa mjini. " Bado tunaendelea kumhoji na ni kweli amekamatwa tupo naye tunaendelea kumhoji ".


Chanzo: JamiiForums
Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.