ZITTO KABWE: NITAMPELEKA ABDUL NONDO UHAMIAJI TAREHE 20/04 KWA MAMLAKA YANGU KAMA MBUNGE WA KIGOMA MJINI


Abdul Nondo Abdul Omar Mitumba, mjukuu wa Marehemu Mzee Omar Mitumba, mwasisi wa TANU na mpigania Uhuru wa Tanganyika leo anaitwa na maafisa Uhamiaji eti kuhojiwa uraia. Hao maofisa uhamiaji na aliyewatuma hawana credentials ambazo Babu yake Nondo, Mwenyekiti wa TSNP anazo. Hii Serikali inatutafuta ubaya.

Wazee wa Ujiji sasa mkae. Tumalize haya mambo ya kipuuzi


Habari zaidi... 

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema Aprili 20 ataongozana na Mwanafunzi Abdul Nondo kupeleka vyeti vya kuzaliwa katika ofisi za Idara ya Uhamiaji kama alivyotakiwa kuthibitisha uraia wake.

Zitto amesema yeye kama Mbunge wa Kigoma ambapo ndipo nyumbani kwa mwanafunzi huyo, ataruhusu wapiga kura wake kumsindikiza ili kuhoji kama Wanakigoma sio Watanzania maana kila mara wamekuwa wakihojiwa juu ya uraia wao. Abdul Nondo alifika Idara ya Uhamiaji mapema leo kuitikia wito ambapo baada ya mahojiano akaamriwa awasilishe cheti chake cha kuzaliwa pamoja na vya wazazi wake ifikapo tarehe 20 mwezi huu.
Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.