SUN TZU NA MASURIA YA MFALME

Sun Tzu alikuwa kamanda wa jeshi na Mwanafalsafa wa kichina enzi hizo china inatawaliwa na maemperor.

Siku moja Sun Tzu akamwambia mtawala (tumwite mfalme) kuwa, mtu yoyote anaweza kuwa mwanajeshi kinachotakiwa ni uongozi mzuri utakaosimamia nidhamu. mfalme huyu alikuwa na jeshi dogo na alikuwa kwenye hatari ya kuvamiwa na ufalme wa jirani.

Basi mfalme akamwambia inamaana hata hawa masuria wangu unaweza kuwafanya kuwa wanajeshi?(masuria kazi yao ilikuwa ni kushinda kujipamba na kujifunza jinsi ya kumridhisha mfalme kingono) Sun Tzu akajibi ndiyo. Mfalme akamwambia hebu nionyeshe. wakaitwa masuria wa mfalme na Sun Tzu akawaonyesha basic moves za mafunzo ya kijeshi. kisha akachagua masuria wawili kuwa kama maofisa watakaoongoza hayo mafunzo. Basi akawaambia ngoma ikipigwa mnaanza mafunzo. Basi ngoma ilivyopigwa wale masuria wakaangaliana na kuanza kucheka.

Sun Tzu akawaambia labda sijaeleweka. akawafundisha tena na kuwaambia ngoma ikilia anzeni mafunzo. Ngoma ilivyolia wale masuria badala ya kujifunzo wakaanza tena kucheka. Sun Tzu akachukua panga kutoka kwa wale masuria viongozi na kuwakata vichwa wale viongozi hapohapo. Kisha akachagua masuria wengine wawili na kuwaambia kuwa ngoma ikipigwa wawaongoze wenzao kwenye mazoezi ya kijeshi.

Basi ngoma ilivyopigwa wale Masuria walifanya onyesho la kijeshi kama vile ni wanajeshi wazoefu wa muda mrefu na wakaa ndani wakijipamba. Basi mfalme akamruhusu Sun Tzu aongoze jeshi lake na aliliongoza kwa mafanikio makubwa.
Image result for animated download now gif
Powered by Blogger.