KAMA UNA STRESS PITIA HAPA! CHEKA UPATE AFYA

Kuna vijimisemo vifupi vimeibuka huku kwenye mitandao kwa sasa, yaani ni full burudani! Ukivisomo mwisho lazima ubaki mdomo wazi au ucheke, baadhi ya niliyokutana nayo naweka hapa, pia karibuni kwa wenye zaidi tuburudike pamoja!

Leo kidogo nipigwe na MWANAMKE baada ya LIFTI kusimama...wakati tupo kwenye lift Nilikua nayaangalia MAZIWA yake akasema "Bonyeza Moja" mi si nikalibonyeza? Yaani had sasa, bado najiuliza nilipokosea.

Hivi Utajisikieje Utakaposikia Rafiki Yako wa Karibu Hajaja Kwenye Mazishi Yako ???! Nadhani Mimi Sitamwongelesha Tena !!!!  I think nakaribia kupona.

Nimenunua chips ili nile kwa bahat mbaya mtoto wa mama mwingine amekaa next to me akaanza kuzililia. 
Imebidi nivae earphones. Napenda watoto, ila utoto ndio sipendi..

Jana nimepita njia ya mkato makaburini warembo wawili wakawa wananikimbilia wanatetemeka Eti tunaogopa kupita peke yetu na mm Nikawajibu hata mm nilivyokuwa hai nilikuwa naogopa sana . Wakazimia. Sipendagi kufatwa fatwa mm


Niliwahi kusikia kuwa maji na mafuta havichangamani, na pia mafuta huwa yanaelea juu ya maji... Basi jana mimi nikaamua kupaka mafuta mengi tu miguuni kisha nikaingia baharini ili niweze kutembea juu ya maji maana nilihisi ningeelea na kuweza kufanya chochote. 
Sikumbuki nini kilitokea lakini nilijikuta nimelala mchangani watu wakiwa wamenizunguka huku wakisema niwashukuru sana wavuvi. 
Nadhani watakuwa wamenipa samaki wa bure.


Leo nimeenda kuchangia damu hospitalini,mara wananambia soda na biskuti zimeisha..! 
Sa hii nipo zangu njiani na damu yangu kwenye blood bag naelekea nyumbani. Bora niwapelekee mbu take away..
.
Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.