NAOMBENI USHAURI: MDOGO WANGU AMEKULA CHENJI YA VIFAA VYA UJENZI, MKE WANGU AMEGUNDUA NA KUMSEMA KWA KEJELI. YUPI ANA MAKOSA?

Naomba ushauri wenu kuna jambo nataka leo nikirudi home niliweke sawa ila inahitajika busara na hekima zaidi kuliko mabavu.


Kuna kibanda najenga huko maeneo ya Chamazi sasa msimamizi wa ujeni ni mke wangu na mdogo wangu wa kiume. Kwenye building estimation cost tulikadiria mfuko wa saruji mmoja utakuwa unauzwa shilingi 15000/= na wakati tunafanya hayo makadirio tulikuwa na huyo bwana mdogo so alijuwa hizo heasbu zetu.

Last week walienda site kuanza ujenzi dogo na wife so wife alimuachia dogo asimamie manunuzi ya saruji na vifaa vya ujenzi . Dogo alipofika dukani alikuta saruji inauzwa shilingi 13500/= so kijana wala hakutoa ushirikiano kwa shemeji yake yeye aliendelea na ile hesabu yake ya shilingi 15000/= mpaka wanamaliza kazi dogo akawa amejilipa shilingi 1500 kwa kila mfuko.

Sasa ijumaa niliacha maagizo watengeneze jiko la ndani waweke sehemu ya kuoshea vyombo katika ile nyumba tunayoishi sio inayotengenezwa. Hivyo dogo alikuwa kwenye mishe zake za kuzurura wife akaona bora akalipie hiyo idadi ya mifuko inayotakiwa ili kijana akirudi atabeba hiyo mifuko kuipeleka home. Ila alipofika kule akakuta bei ya mfuko mmoja ni shilingi 13500/= mke wangu kwa sababu ni mchumi sana na ni watu wanaoishi jirani na Paul Kagame na mwenzie Nkurunzinza alisikia hasira sana akaona dogo amempiga changa la macho.

Kufanya habari isiwe ndefu wife alimpgia simu dogo then akamfokea sana tena kwa maneno ya kejeri na dharau dogo alisubiri nilivyorudi akanieleza issue ilivyo wala sikumjibu kitu nikasubiri usiku nikaongea na wife naye akawa mbogo hivyo nilimuuliza tu hivi wewe na mimi nani aliyetafuta hizo hela? Huyu dogo kama amekula hela si amekula za kaka yake wewe kinachikuuma ni kitu gani?

Sasa sijapata suluhu kwa mke wangu kwa sababu ya hilo jambo ukizingitia sipendi migogoro ya aina hii ipate nafasi ndani ya nyumba yangu. 

Je nifanyaje ili niweze kuwaweka sawa hawa watu ili tuishi kwa amani kama ilivyokuwa mwanzo?!..

Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.