TANZIA: AMRI ATHUMAN (KING MAJUTO) AFARIKI DUNIA KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI

TANZIA: Msanii wa vichekesho Mzee King Majuto amefariki dunia usiku wa leo Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu. Msemaji wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha amesema Mzee Majuto alipelekwa hospitalini hapo Julai 31 baada ya hali yake kubadilika.

“Hali yake ilibadilika majira ya saa tisa alasiri ya leo hivyo kuhamishwa kutoka jengo la Sewahaji kwenda ICU. Ilipofika saa 1.30 jioni hii hali yake ilibadilika zaidi na madaktari walijitahidi kuokoa maisha yale bila mafanikio. Ilipofika saa 2 usiku alikata roho,''

Pia soma >
--
Wasifu
Amri Athuman’ King Majuto’ alizaliwa mwaka 1948 jijini Tanga na kusoma shule Msambwini, Tanga, alianza kuigiza 1958 akiwa na umri wa miaka 9 akiigiza katika majukwaa Mzee Majuto maarufu kama King Majuto ni mtunzi, muigizaji,mwandishi wa mswada.

Na ndiye muigizaji wa kwanza kuandaa kazi zake katika mikanda na kuuza akiwa na Tanzania Film Company ( TFC) Kwa sasa King Majuto ni mwigizaji mwenye mashabiki wengi kutokana maonyesho mbalimbali, vichekesho vyake aliyoshiriki nchi mbalimbali.

Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.