HIZI NDIZO SABABU KWANINI WEWE UNANUNUA UMEME KWA BEI KUBWA TOFAUTI YA WENGINE


Umesha wahi kujiuliza kwa nn wewe unanunua umeme kwa bei kubwa tofauti na jirani yako au rafiki ako yy akinunua umeme wa 5000 anapata unit 41 huku wewe elf 5000 hiyo hiyo unapata unit 14 tu 10,000 unapata unit 28 wakati wenzako 9150 wanapata unit 75!?

Majibu haya hapa, kuna hii ya watumiaji wadogo wa umeme ambayo kwa mwezi unatakiwa usiwe unatumia unit zaidi ya 75 kwa miezi mitatu au 6 mfululizo ndipo unaenda Tanesco kuomba kupunguziwa matumizi ya gharama za umeme yaani kushushwa tarifu kutoka 1 kwenda 4 ambayo unauziwa unit 1 kwa sh 122 wakati ile ya tarif 4 ambayo wengi ndo wapo unauziwa unut 1 kwa 355 maana yake hapa ukiwa ukinunua umeme wa 1000 unapata unit2 na point 3 hazifiki 5000 unit 14 na point 10000 unit 28 lakini ukiwekwa tarif 4 ya watumiaji wadogo wa umeme 500 unapata unut 4 na ponit 1000 unit 8na point 2000 unit 16 na point 5000 unit 41 na 9150 unapata unit 75 ambazo hizi hutakiwi kuzidisha ukizidi tu imekula kwako unahamishwa tarif automatical hapa lazima uwe makini sana

na kama ni nyumba ya kupanga sio rahisi ila kama umeka pekee yako nyumba nzima Unaweza maana hata mimi ndio ninaotumia kwa mwezi sifikishi hata unit 60..NB kama unajua huwezi kujibana ukatumia unit 75 tu kwa mwezi mzima basi huduma hii hikufai maana hata ukiwekwa kweny taarif hii ukizidisha unit 75 kwa mwezi wanakuondoa unawekwa tarif 1.. Kuna watu wanaweza kuuliza unafanyaje ili upunguze matumizi ya umeme ili kwa mwezi usizid unit 75 jibu ni kupunguza matumizi ya umeme yasiyo ya lazima kama kutoa taa au bado barunu zenye wati nyingi na kubwa ukaweka taa zenye wati kidogo mfano mimi nikikuwa natumia taa zenye wats 40 zilikuwa 4 nje na za wats 18 ndani kwenye vyumbani na sebreni taa 8 nyumba nzima zilikuwa taa 12 na ilikuwa jumla ya wats 304
ikizidisha hapo bado feni na friji nk ila now baada ya kuweka taa zenye wats kidogo nje niweka zenye taa zenye wats 5 tu na zina mwanga mkbuwa unanitosha japo zinauzwa bei kubwa pia kwa vyumbani niweka za wats 3 now nyumba nzima taa ina taa 12 zile zile ila now zina jumla ya wats 44 zote wakat hapo mwanzo kabla cjazibasilisha ilikuwa wats 304 ona hapo kwenye upande wa taa tu nilivosave wati zaidi ya 250 kwa hiyo wewe ukiwasha taa yako moja yenye wats 40 na mimi nikawasha taa 12 za nyumba yangu yote tunalingana matumizi wewe taa 1 wati 40 mimi taa 12 wai 44 unaona hapo.. Ngoja niishie hapo nisiwashoshe sana hapo bado radio zenye wats kubwa na ndogo ,firiji pia kuna zinakula sana umeme na ambazo hazili kabisa kwa hiyo ni vizur kila kifaa unachotumia ukijue kinatumia umeme kiasi gani na kiwa wats ngapi

Mimi sio mtaalam wa mambo ya umeme hata kidogo ni raia wa kawaida sana na nmewahi kutumia unit 4 kwa siku 1 na kwa mwezi unit 120 kwa miaka mingi ila baada ya kuona kuna majirani zangu wenye nyumba ya ukubwa kama yangu na vifaa sawaa na vyangu nimekuwa mchunguzi sana nikaanza kufuatilia kwa kuwauliza wao walifanyaje mpaka wakapunguziwa nk ndio na mimi nikafuata haya niliyowaeleza hapa nakafanikiwa kubadilishiwa tarif now nakula raha pia ninachunguza na kiangalia kila kifaa nnachotumia najua kina wats ngapi hata kabla sjakinunua naangalia nikuta kina wats nyingi huwa naachana nacho na kutafuta chenye wats ndogo hata kama kinauzwa bei kubwa nanunua. Na mara nyingi vifaa vyenye wats ndogo vinauzwa bei kubwa zaidi ukilinganisha na vyenye wats kubwa mfano kuna taa zile za kizamani zenye wats 200 au 100 zinauzwa 500 tu wakati kuna taa zenye wats 3 onauzwa 4000 na wats 5 inauzwa 5000 unaona hapo sasa unanunua bei kubwa inakuja kukusave kwenye matumizi, unanunua bei. Ndogo unakuja kukukost kwenye matumizi ya umeme..

Kama kuna mwingine kutaka kuongizea aongezee hapo nikipoishia Mimi karibuni tuelimishane hakuna anaejua kila kitu ndio maana kila siku tunajifunza..nipo tayar kumuelekeza kila mtu anaehitaji ushauri na mbinu mbalimbali ili aweze kubana matumizi na mpka kuweza kubadilishiwa tarif na tanesco. .kumbuka hata ukifungiwa au kuunganishwa umeme leo unawekwa tarif 1 ili ubadilishwe tarif 4 mpka uone matumiz yako ya umeme yakoje na uende tanesco uandike barua ya kuomba kubadilishwa.. Ukikaa kimya hata hata kama unatumia kwa mwezi unit 30 tu hautabadilishiwa tarif so lazima ukaombe.

Chanzo: JamiiForums


Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.