BAADA YA KUSHINDWA NA JOYNER LUCAS, TORY LANEZ ANATAFUTA BIFU JIPYA NA ROYCE DA 5'9

Kuna kitu Tory Lanez anakitafuta na bila shaka atakipata muda si mrefu, kwanza alianza na kumdiss Joyner Lucas na akaambulia michano ya haja kiasi kwamba akajikuta anapoteza mpambano wake na Joyner. Jana ameibukia kwa Royce Da 5'9 baada ya mtu kumuuliza Royce kwenye twitter kama Tory Lanez alishinda kwenye bifu lake na Joyner. Kwa neno moja tuu, Royce alimjibu 'NO' kitu ambacho kilionekana kumkera Tory na kujikuta amemjibu maneno machafu Royce. Unahisi hii ni bifu nyingine ambayo tunafunga nayo mwaka 2018?

Image result for animated download now gif
Powered by Blogger.