KWANINI VIJANA WA SIKU HIZI WANAISHI MAISHA YA MAIGIZO?!

Najua wengi mtakubaliana na mimi kwamba vijana walio wengi siku hizi wanaishi maisha ya maigizo kwa mfano mimi nina marafiki zangu nawajua vizuri lakini:


1. Kuna mmoja huyo anapenda kujifanya anafanya mtu wa usalama wa Taifa.

2. Kuna jamaa yangu mmoja kaishia la saba lakini huwa anajifanya msomi ana degree toka udsm.

3. Mwingine huyo kila siku huwa anapenda kupiga picha sehemu nzuri nzuri kwenye magari ya watu, anajipiga picha yupo ofisini kwa watu kisha anatupia facebook kisha anawekaga status sijui on my office kumbe mishen town.
4. Kuna mmoja yeye anajifanya yupo Ikulu anajifanya anafanya kazi basi ukimsikiliza story zake anajifanya anaijua nchi.

5. Yupo mmoja anajifanya ana hela anapenda piga picha mezani bia zimejaa anajiita boss man kumbe hana kitu.

Nina mifano mingi lakini twende mbele turudi nyuma ivi kuna faida gani mtu kuishi maisha ya maigizooo kuna faida gani.
Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.