NIMEKOMA KUKAGUA SIMU YA MUME WANGU!

Habari za usiku huu waungwana.. naamini wote mko salama.
Niwaambie yaliyonikuta sasa.. week kama tatu zilizopita nilianza kuhisi mume wangu anakimada ila sikutaka kumuuliza wala sikutaka ajue kama nahisi anachepuka. Mumewangu alikua na tabia ya kuwahi kurudi nyumbani au hata kama anajua anachelewa hua lazima apige simu kunitaarifu.

Mumewangu alikua amenipa Uhuru na simu yake hata kama anaoga alinipa ruhusa niipokee na niongee na mpigaji na sio tu mimi Uhuru huo aliwapa hata watoto wake. Wiki tatu zilizopita nikaona mwenzangu ameanza kubadilika..hatuna ruhusa ya kushika simu..hata kama inaita atatoka bafuni na apovu lake ataichukua simu maongezi yatafanyika bafuni..ukali ukaanza kwangu na watoto hata kama haikua na haja ya kutukalipia.

Nikaanza kufuatilia mwenendo wake ndipo nilipogundua ana mwanamke..leo asubuhi nikasubiri ameenda kuoga nikachukua simu bahati nzuri nywila yake naifahamu nikapunguza sauti nikaanza kupekua kwenye whatsapp. Nikakutana na picha za tupu za huyo mwanamke huku wakisifiana wanavyofurahishana kitandani..nilijikuta sina nguvu kwakweli..ghafla na yeye akatoka bafuni akavaa huyo akaondoka hata kifungua kinywa hakupata.

Muda wa kama nusu saa hivi nikamtumia meseji 

Mimi: "Ahsante nimeona na nimejua kila kitu"
Mume wangu: "Umekipata ulichokua wakitafuta na ukome"
Mimi: "Yani Mume wangu ndio wanijibu hivyo?"
Yeye: "Tena umenikera na sirudi Leo"

Yani ninavyoandika hapa hadi sasa 11:36pm huyu mwanaume bado hajarudi na simu yake haipatikani. Wanawake wenzangu naomba mnishauri nifanye nini?

Wanaume mnahisi alichokifanya mwanaume mwenzenu ni sahihi?

No comments

Powered by Blogger.